Mshambuliaji wa Manchester City Gabriel Jesus anahusishwa na kujiunga na Arsenal katika msimu ujao.
Jesus, mwenye miaka 25, amebakisha mwaka mpya wa kuitumikia Manchester City.
Hata hivyo, amekanusha habari hiyo na kusema hana mpango wa kuhama.
Mwezi uliopita alifunga magoli 4 dhidi ya Watford na kuzidi kuonyesha umuhimu wake klabuni hapo.
Tetesi za Jesus kuondoka Etihad zinakuja baada ya Man City kumvuta Erling Haaland kutokea Borrusia Dortmund ya Ujerumani.
“Tumeongea na Arsenal kuhusu kumchukua Jesus,” amesema wakala wa mchezaji huyo.
” Kuna klabu nyingi zinamuhitaji, lakini kwa sasa nguvu yake yote bado ipo katika mechi zilizobaki za kumaliza msimu,” amenukuliwa wakala wake.
Habari za ndani zinasema Arsenal wamepata nguvu ya kumshawishi Jesus kuhamia klabuni hapo baada ya Man City kusuka vizuri mpango wake na Haaland.
Kocha wa Arsenal Mikel Arteta aliwahi kumfundisha Jesus wakati alipokuwa kocha msaidizi wa Man City chini ya Pep Guardiola.
The post Arsenal yataka kumng’oa Jesus Man City first appeared on KITENGE BLOG.
The post Arsenal yataka kumng’oa Jesus Man City appeared first on KITENGE BLOG.
By Author
Post a Comment