Marekani imesema staa wa movie ya ‘Hotel Rwanda’ aliyefungwa kwa makosa ya ugaidi nchini Rwanda alikamatwa kimakosa.
Staa huyo Paul Rusesabagina anaonekana katika filamu hiyo akiwapa chakula mamia ya watu wakati wa vifo vya mauaji ya kimbali yaliiyotokea nchini Rwanda mwaka 1994.
Rusesabagina, mwenye miaka 67, alihukumiwa mwezi Septemba uliopita kwenda miaka 25 jela kwa makosa 8 ya ugaidi.
Inasemekana ni mkosoaji mkubwa wa serikali ya Rwanda.
Hivyo, inadaiwa kuwa kifungo hicho kinatokana na kupinga kwake utawala wa Rais Paul Kagame wa nchi hiyo.
Hata hivyo, amekana mashitaka yote yaliyokuwa yanamkabili.
Lakini amekubali kuwa kiongozi wa chama cha kupigania demokrasia nchini humo ( Rwanda Movement for Democratic Change-MRCD).
Marekani ina amini haki haijatendeka kwa staa huyo.
Hivyo inadai kesi hiyo ina mkono wa kisiasa.
The post Marekani yadai staa wa movie ya ‘Hotel Rwanda’ amefungwa kimakosa first appeared on KITENGE BLOG.
The post Marekani yadai staa wa movie ya ‘Hotel Rwanda’ amefungwa kimakosa appeared first on KITENGE BLOG.
By Author
Post a Comment