MBUNGE KUNAMBI AKABIDHI SH MILIONI 500 KWA VIKUNDI VYA WAJASIRIAMALI MLIMBA |Shamteeblog.


MBUNGE wa Jimbo la Mlimba, Godwin Kunambi amekabidhi hundi ya Sh Milioni 500 kwa vikundi 44 vya Wanawake na Watu wenye Ulemavu pamoja na Pikipiki 52 zenye thamani ya Sh Milioni 135 kwa vikundi 44 vya vijana katika Halmashauri ya Mlimba. Fedha hizo ni mikopo inayotokana na asilimia 10 inayotolewaga na Serikali kwa makundi hayo matatu.

Akizungumza baada ya kukabidhi Hundi na Pikipiki hiyo, Mbunge Kunambi ameishukuru Serikali ya Rais Samia kwa namna ambavyo imekua mstari wa mbele katika kuinua maisha ya Wanawake, Walemavu na Vijana kupitia mikopo hiyo ya asilimia 10 ambayo hutolewa na Halmashauri.

"Miezi mitano nyuma tulikabidhi Sh Milioni 918 na Pikipiki 20 kwa vikundi vya Wanawake, Walemavu na Vijana, leo hii tunayo furaha katika Jimbo letu la Mlimba kukabidhi Sh Milioni 516 na Pikipiki 52 zenye thamani ya Sh Milioni 135, kwetu hii ni hatua kubwa sana ya kuzidi kuyainua makundi haya matatu kwa kuhakikisha yananufaika na mikopo hii isiyo na riba inayotolewa na Serikali kupitia Halmashauri zetu.

Niwaombe Ndugu zangu mliopata mikopo hii, nendeni mkaifanyie kazi vizuri ili muweze kulipa marejesho yenu bila usumbufu, kwa kufanya kazi kwa bidii mtakua mmemuunga mkono Rais Samia ambaye Serikali yake ndio inayotoa mikopo hii isiyo na riba.

Nitoe wito kwa maafisa Biashara, Maafisa Ugani kutembelea vikundi hivi mara kwa mara ili kutoa ushauri wa kitaalamu waweze kufanya biashara zao vizuri, tusikae ofisini tu tusaidienj kuwafuata hawa wajasiriamali wanaopata mikopo hii na kuwapa elimu,," Amesema Kunambi.

Amesema ataendelea kushirikiana na Halmashauri kuhakikisha wanaweka miundombinu bora kwa vikundi vinavyokidhi vigezo kuweza kupatiwa mikopo hiyo huku akiwaasa kuirudisha kwa muda waliopangiwa ili wengine wenye sifa waweze kupatiwa mikopo hiyo.







 

By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post