Mvua ya magoli imetawala baada ya wenyeji Namungo FC kulazimishwa sare ya kufungana mabao 3-3 na Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Ilulu mjini Lindi.
Haruna Shamte alitangulia kuifungia Namungo goli la mapema dakika ya 5 kabla ya Ezekia Mwashilindi kusawazisha dakika tatu baadae.
Jumanne Fadhili aliifungua Polisi goli la pili katika dakika ya 55 kwa njia ya penati.
Nurdine Chona alijifunga dakika ya 65 na kuipa Namungo goli la pili.
Moses Kitundu aliifungia Prisons goli la tatu dakika ya 77 kabla ya Lucas Kikoti kuifungia Namungo dakika ya 86.
Kwa matokeo hayo, Namungo wanafikisha pointi 37 na kuendelea kushika nafasi ya tatu, wakati Tanzania Prisons wanafikisha pointi 24 na kusogea kwa nafasi moja juu hadi ya 14 baada ya wote kucheza mechi 25.
The post Namungo, TZ Prisons waonyeshana ubabe first appeared on KITENGE BLOG.
The post Namungo, TZ Prisons waonyeshana ubabe appeared first on KITENGE BLOG.
By Author
Post a Comment