Serikali yatilia mkazo wa kudhibiti Malaria nchini-Dk.Sichalwe |Shamteeblog.



*Maabara ya kisasa ya kufatilia Vinasaba uchunguzi wa malaria yasimikwa NIMR

Na Chalila Kibuda, Michuzi Tv

Serikali imeweka mkazo katika kudhibiti malaria kwa kwa kuendelea kutafiti ugonjwa huo kina katika kuwa na maabara ya kisasa ya kufatilia Vinasaba ya uchunguz.

Hayo ameyasema Mganga wa Mkuu wa Serikali Dk.Aifello Sichalwe kwa niaba ya Waziri wa Afya wakati akifungua Maabara ya Vinasaba Uchunguzi wa Malaria Jijini Dar ee Salaam, amesema serikali awamu ya Sita kupitia Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa Binadamu (NIMR) na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Tawala za Serikali (TAMISEMI) imeweza kupata mradi wa Bill &Melinda Gates wa maabara ya kisasa ya uchunguzi wa Vinasaba kufatilia ugonjwa wa Malaria

Amesema maabara hiyo pia itafanya ufutatiliaji wa kusaidia katika mikoa 13 katika kufatilia vinasaba vya ugonjwa wa malaria ambayo ina viwango vikubwa cha malaria.

"Tunashukuru Bill &Melinda Gate kwa mradi na hata ukiisha waendelee kufadhili kutokana kuanzisha maabara hii katika kulinda wananchi"

Dk Sichalwe amesema Wizara kupitia mpango wa Taifa wa kudhibiti Malaria imeweka mpango wa ufutatiliaji wa ugonjwa huo ili kuangamiza.

"Maabara hii itakuwa na Msaada mkubwa kwani mpango wa Taifa wa malaria utaitumia kufatilia ugonjwa huo na kupata na ushahidi wa utafiti utatolewa katika maabara hiyo" amesema Dk. Sichalwe.

Amesema Serikali imeendelea kupamba na magonjwa kupitia mpango wa malaria hivyo sasa watafatilia kwa njia ya kisasa kutokana na kujua kwa teknolojia.

Alibainisha kuwa mradi huo ulianza mwaka mwezi Mei 2020 na inatarajiwa kukamilika mwaka 2023.

Dk Sichalwe alisema utafiti unaendelea kufanyika katika mikoa 13 ambayo ni Dar esSalaam,Tanga,Tabora,Songwe,Dodoma,Manyara,Njombe,Ruvuma,Kagera,Kigoma,Mara na Mtwara.

"Na Waganga wa mikoa wamehusika na mradi umefadhiliwa na Taasisi ya Melinda and Billgate tumekaa kuzungumza waendelee kufadhi hata wadau wengi lengo tutokomeze ugonjwa .

"Maabara hiyo sasa inafanya kazi Itapima na kuchakata vina saba na sisi tutatumia katika kuandaa sera na mipango katika kupambana na magonjwa,"amesema.

[Aidha, Dkt Sichalwe ameendelea kufafanua kwamba utafiti huo utasaidia kuwajengea uwezo NIMR Kwa kuzalisha takwimu za vinasaba vya Maleria hapa Nchini nakuzichakata kisha wizara ya afya itazitumia kufanya maamuzi ikiwemo kuandaa miongozo, kutunga sera nakutekeleza mikakati mbalimbali yakupambana na malaria huku wakiwa na ushahidi wa kisayansi.

Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri Taasisi ya Utafiti wa magonjwa ya Binadamu ( NIMR) Dk. Khadija Malima amesema kwamba utafiti wa vinasaba vya ugonjwa wa malaria utekelezaji wake umeanza tangu Mwezi Mei 2020 na inatarajiwa kukamilika mwezi oktoba 2023 ambapo kwa sasa umeanza katika mikoa kumi na tatu Nchini kote.

Dk.Khadija ameongeza kwamba wasimamizi wakuu wa utafiti huo wa vinasaba vya malaria ni waganga wakuu wa mikoa pamoja Afisa afya.

Aidha maabara imeshakamilika na inaenda kufanya kazi iliyokusudiwa ili kusaidia kuleta suluhisho la ugonjwa huo ambao umekuwa ukipoteza idadi kubwa ya watu

Hata hivyo, Serikali imesema itahakikisha inaongeza jitihada za kutokomeza ugonjwa wa malaria ambao umekuwa tishio na kusababisha vifo vya watu wengi kila siku.
Mganga Mkuu wa Serikali Dk.Aifello Sichalwe akikata utepe kuashiria uzinduzi wa maabara ya kisasa ya Vinasaba uchunguzi wa Malaria katika Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), jijini Dar es Salaam.


Mganga Mkuu wa Serikali Dk.Aifello Sichalwe akizungumza wakati wa uzinduzi wa maabara ya kisasa ya Vinasaba uchunguzi wa Malaria katika Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), jijini Dar es Salaam.




Wataalam wakiwa na sampuli katika maabara wakitafiti


Mganga Mkuu wa Serikali Dk.Aifello Sichalwe akizungumza wakati wa kuhusiana na uwezo wa maabara ya kisasa ya Vinasaba uchunguzi wa Malaria katika Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), jijini Dar es Salaam.

Mganga Mkuu wa Serikali Dk.Aifello Sichalwe akipata maelezo kutoka Mtafiti Mkuu na Kiongozi wa Mradi wa Maralia wa NIMR Dk.Deusdidith Ishengoma kuhusiana na maabara ya kisasa ya Vinasaba uchunguzi wa Malaria iliyozinduliwa katika Taasisi ya NIMR jijini Dar es Salaam.






By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post