Wadau katika sekta ya afya wapongezwa kwa mchango wao katika ufanikishaji wa Huduma ya Afya kwa Wote |Shamteeblog.

Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango akizungumza wakati akifungua Kongamano la 31 la Kisayansi lililoandaliwa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadam (NIMR) liliofanyika jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Mradi wa HPSS Ally Kebby akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Mradi huo namna walivyoka mifumo mbalimbali ya utoaji wa huduma za afya katika vituo vya afya wakati wa Kongamano la 31 la Kisayansi lililoandaliwa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadam (NIMR) liliofanyika jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango akipata maelezo ya mradi wa HPSS  kutoka kwa Mshauri wa uwezeshaji Fedha za Afya wa Mradi wa HPSS Elizeus Rwezaula  wakati alipotembelea Banda la Mradi katika Kongamano la 31 la Kisayansi lililoandaliwa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) lililofanyika jijini Dar es Salaam.
Wadau wa sayansi wakiwa katika Kongamano la 31 ya Kisayansi lillofanyika jijini Dar es Salaam.
Picha ya Pamoja Mgeni Rasmi Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango pamoja wafadhili wa Kongamano la 31 la Kisanyansi lililoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu(NIMR) , jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu 

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Phillip Mpango amewapongeza wadau wa sekta ya afya nchini kwa jitihada zao mbalimbali zinazochangia owezekano wa kufikia azma ya serikali ya kufanikisha utolewaji wa huduma za afya wa wananchi wote ifikapo mwaka 2030.

Dk Mpango ameongea haya wakati akifungua Mkutano wa 31 wa Kisayansi ulioandaliwa na Taasisi ta Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), kwa kushirikiana wa wadau mbalimbali wenye kauli mbiu "Mbinu shirikishi katika ya Afya: Ajenda ya Kuimarisha Mifumo ya Afya Katika Kuelekea Kufikia Huduma ya Afya kwa Wote".

Kaulimbiu hiyi ni muhimu na imekuja kwa wakati kwa Tanzania huku Jumuiya ya afya duniani ikisisitiza kwamba ili kufikia huduma ya afya kwa wote, kuna haja ya kuimarisha mifumo ya afya ya nchi na pia kuboresha uratibu wa juhudi na mipango.

Akizungumza na washiriki, Dk Mpango amesema mkutano huo umefanyika katika kipindi ambacho taifa linakumbana na changamoto mbalimbali za kiafya ambazo zinahitaji ufumbuzi wa kisayansi, kama vile Uviko -19 na magonjwa yasiyiambukizwa ambayo yanasababisha zaidi ya asilimia 70 ya vifo duniani.

 “Mkutano huu ni fursa ya kipekee kwa wanasayansi wa Tanzania kujifunza kutoka kwa kila mmoja na kuunganisha werevu na uwezo katika kupata masuluhisho ya msingi kwa changamoto kuu za kiafya hapa nchini”

Mradi wa HPSS- Tuimarishe Afya, unaofadhiliwa na Serikali ya Uswisi na kutekelezwa na Taasisi ya Swiss Tropical and Public Health Institute ni mmoja wapo wa wafadhili wa mkutano huo na mshirika mkuu katika afua za uimarishaji wa mifumo ya afya nchini tangu 2011.

"Tunafanya kazi na Serikali kupitia Ofisi ya Rais – TAMISEMI na Wizara ya Afya katika kutengeneza masuluhisho ya kiubunifu kuhusu, mifumo na sera za kitaifa. Tumejielekeza zaidi katika kuboresha mfumo wa afya, upatikanaji, matumizi na ubora wa huduma za afya nchini Tanzania”, alisema Ally Kebby, Meneja wa Miradi wa HPSS Tuimarishe Afya.

Katika Mkutano huo wa siku tatu, Mradi wa HPSS Tuimarishe Afya utatoa mawasilisho kadhaa yanayoangazia uimarishaji wa mifumo ya afya katika kuelekea kufikia huduma ya afya kwa wote kwa kuhamasisha umuhimu wa bima ya afya na usambazaji wa bidhaa za afya.

Pamoja na hayo, Mradi wa HPSS Tuimarishe Afya utawasilisha matokeo ya utafiti yanayohusiana na mipango yake - chini ya kauli mbiu: "Bima ya Afya ya CHF Iliyoboreshwa, kuleta mabadiriko katika uliokuwa mpango wa malipo ya kabla, kuwa Bima kamili ya Afya ya Jamii”.

Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Bunadamu (NIMR) imekuwa ikiandaa mikutano ya Kisayansi kama huu tangu 1982 ambapo wadau mbalimbali wanaojumuisha watafiti, wanataaluma, wasimamizi wa afya, wanafunzi, viongozi wa Serikali, Wanahabari na wawakilishi wa makundi maalum hushiriki na kujadili matokeo ya tafiti za afya, mbinu bora na kutambua maeneo muhimu yanayohusiana na afya ambayo yanahitaji hatua za haraka.



By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post