Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Mteja wa Shirika la Taifa la Bima (NIC)Yesaya Mwakifulefule akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuhitimishwa kwa mbio za Korosho Marathon zilizofanyika katika Kiwanja Cha Nagwanda Sijaona leo mkoani Mtwara.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Zainab Telack akimkabidhi kikombe cha Ushiriki wa Korosho Marathon Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Mteja wa Shirika la Taifa la Bima (NIC ) Yesaya Mwakifulefule leo katika Kiwanja cha Nagwanda Sijaona mkoani Mtwara.
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV Mtwara
MKURUGENZI wa Masoko na Huduma kwa Mteja wa Shirika la Taifa la Bima (NIC) Yesaya Mwakifulefule amesema kuwa Korosho Marathon ni aina yake kutokana kuwa wadau wengi kuliko marathon zilizopita.
Mwakifulefule amesema hayo mkoani Mtwara wakati Korosho Marathon iliyofanyika katika Viwanja vya Nagwanda Sijaona mkoani humo.
"NIC imekuwa sehemu ya wadhamini kutokana kutambua michezo na ndio wadau wa bima kwa kukata katila mahitaji yanayohusian a na Bima"
Amesema kuwa michezo ya mbio ina imarisha afya kwa wakimbiaji na kuwa na nguvu kazi ya taifa inahitaji wa watu wenye afya.
Mwakifulefule amesema kuwa NiC inatambua umuhimu wa mbio ndio maana tumekuwa wadau katika kudhamini.
Aidha amesema NIC ni shirika kubwa limeendelea kutoa elimu ya bima na zao la korosho kwa wa sasa lina bima la unyaufu ambapo imepunguza kilio cha wafanyabiashara wa korosho.
Mkurugenzi Masoko na Huduma na Huduma na huyo ameeleza kuwa NIC iko katika soko la bima hivyo litaendelea kuwafikia wadau kwenye bima kwani mahitaji ni mengi.
Picha ya pamoja ya wadau wa Korosho Marathon wakiwa na Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Mteja Yesaya Mwakifulefule kwenye korosho marathon zilizofanyika mkoani Mtwara.
Picha mbalimbali kwenye bango Ukuta wa NIC kwenye Korosho Marathon
By Mpekuzi
Post a Comment