Bilioni nne na milioni 264 zakarabati Nyumba JWTZ Mwenge Dar, Dkt. Stergomena apongeza |Shamteeblog.

WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) amelipongeza Jeshi la Wananchi (JWTZ) kwa kuwa wabunifu wa kukarabati nyumba za kuishi wanajeshi wa jeshi hilo kwa gharama nafuu.

Ametoa pongezi hizo mara baada ya kukagua Maghorofa ya Mwenge jijini Dar es Salaam leo Agosti 19, 2022 amesema kuwa ukarabati huo ni wakuigwa mfano.

Amesema kuwa kazi kubwa imefanyika katika kukarabati na kuboresha makazi hayo na sio kazi ndogo kwa kutumia kiasi cha shilingi bilioni nne na Milioni 264 kwa majengo 14 ni kitu cha kupongezwa na kuigwa.

Amesema Mpaka sasa wamefikia asilimia 65 ya kukarabati maghorofa hayo ambapo katika asilimia hizo imetumika shilingi bilioni mbili na milioni 156 tuu.

"Kwa fedha hizo zingeweza kujenga jengo moja tuu, jeshi letu mmeuishi wito wetu wa utii, Uhodari na Uaminifu hii ndio inajionesha wazi kweli mmekiishi kiapo chenu." Amesema Dkt. Stergomena

Pia ameupongeza uongozi wa Jeshi kwa kuona umuhimu wa wataalamu waliopo katika jeshi hilo badala ya kuweka mzabuni ili akarabati majengo hayo. 

Nimefurahi zaidi ule ubunifu kwamba hata pale ambapo mliona hatuna uwezo wa ndani kwa kutumia wanajeshi wetu, tumewatumia vizuri zaidi kujenga uwezo wetu wenyewe, kwahiyo nawashukuru na ninawapongeza sana...."

Ikiwa ni jitihada za serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais na Amiri Jeshi Mkuu Samia Sulu hassan kuona kazi inayofanyika hapa Mwenge na inachangia vipi kupunguza hii kero ya makazi kwa wanajeshi na tunaweza kuiga nini katika kazi hii na tunaweza kuiga nini kufanya kazi nyingi zaidi.

Amesema ubunifu kama huo utawezesha kupunguza gharama na kuweza kujenga majengo mpya. 

Amesema kuwa kazi ya ukarabati wa majengo hayo ni kuwapa hamasa maafisa na maaskari ili watambue kwamba serikali ipo, Uongozi wa Jeshi la Wananchi upo, unatambua mahitaji yao, unatambua changamoto zao na Unazifanyia kazi.

Akizungumzia wale wanaozani kuwa Maghorofa ya JWTZ yamebinafsishwa amesema kuwa "Huu ni Uhalisia kwamba hapa bado ni makazi ya Maaskari na maafisa wetu na ni kazi inayofanywa kwa mikono ya wataalamu na watendaji kutoka Jeshi la Ulinzi Wananchi wa Tanzania.

Licha ya hayo amewaasa kukamilisha Nyumba hizo kwa muda ambao walijipangia ili nguvu  iliyopo na utaalamu huo waendelee kuutumia sehemu nyingine kwani wanamambo mengi ya kufanya.

Kwa Upande wa Mkazi wa Maghorofa ya JWTZ, Warda Elisante ameishukuru Serikali  kwa kuwakarabatia Makazi hayo sasa yamekuwa mazuri kwa binadamu kuishi.

"...Yaani kwa sasahivi tunakaa ndani tuu kwa uzuri wa nyumba hizi hatutamani hata kutoka nje kwa jinsi walivyotukarabatia vizuri, tunawashukuru sana sasa hivi ni tofauti na mwazo."Amesema Warda

Pia amewaasa wakazi wa Majengo hayo kuzitunza nyumba hizo vizuri pamoja na mazingira yanayowazunguka.

Kwa Upande wa Bethania Dikson amemshukuru Rais Samia, Waziri wa Ulinzi Stergomena na aliyekuwa Mkuu wa Majeshi, Venance Mabeyo kwa kuwakumbuka wakazi hao. 

Kwa sasa hivi Nyumba zetu zinamabadiliko ndani ni kusafi tunakokaa, kwa sasa tunaoga maji kwa kutumia shower." Amesema Berthania

"Kwa sasa hata waumezetu wakiwa wanaenda kazini wanajisikia kwa sababu mazingira ni mazuri, kipindi kile tulikuwa tunatia aibu, sasa hivi tupo vizuri kwa kweli......"
Maghorofa ya  JWTZ ya Mwenge jijini Dar es Salaam ambayo yamesha karabatiwa.
Majengo ya Ghorofa ya Mwenge jijini Dar es Salaam ambalo bado halijakarabatiwa.


Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) akiwa katika picha za pamoja wa wafanyakazi pamoja na wakazi wa Majengo ya JWTZ ya Mwenge jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) akizungumza mara baada ya kutembelea na kukagua na kujionea namna ukarabati wa maghorofa ya JWTZ ya Mwenge jijini Dar es Salaam yalivyofanyiwa ukarabati.
Mkazi wa Maghorofa ya JWTZ, Warda Elisante akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Agosti 19, 2022 akishuhudia namna ambavyo wamependezwa na ukarabati wa nyumba za kuishi wafanyakazi wa JWTZ pamoja na familia zao.
Bethania Dikson akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Agosti 19, 2022 akishuhudia namna ambavyo wamependezwa na ukarabati wa nyumba za kuishi wafanyakazi wa JWTZ pamoja na familia zao.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) akitemebela ukarabati wa maghorofa ya JWTZ ya mwenge jijini Dar es Salaam leo Agosti 19, 2022.


By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post