Chuo Kikuu cha Oxford nchini Uingereza kinatarajiwa kuanza kufanya majaribio ya dawa aina ya vidonge iliyoitafiti kwa ajili ya kupambana na ugonjwa wa Monkeypox.
Ugunduzi wa dawa hii ya majaribio unakuja huku kukiwa na taarifa kuwa zaidi ya watu 3,000 nchini humo wamepata na ugonjwa huo.
Virusi hivyo, ambavyo vinatapakaa kwa kasi sana duniani, tayari vimetangazwa kuwa janga la dunia.
Mtu mwenye virusi hivyo anaweza kumwambukiza mtu mwingine aliye karibu naye.
Na anayepatwa na virusi hivyo huchukua wiki kadhaa kupona na huenda akajikuta anaingia katika matatizo mengine ya kiafya.
” Lengo ni kuwasaidia wale wote wanaopata changamoto ya virusi hivi,” amesema Profesa Sir Peter Horby.
Katika majaribio ya dawa hiyo inayoitwa ‘ Tecovirimat’, watu wapatao 500 watafanyiwa majaribio hayo ili kuangalia kama dawa hiyo itafanya kazi vizuri.
Tecovirimat, au kwa jina lingine Tpoxx, inafanya kazi ya kuzuia virusi vya ugonjwa huo kusambaa katika mwili na imepewa leseni kwa ajili ya kuzuia ugonjwa huo baada ya kufanyiwa utafiti kwa wanyama.
The post Dawa za kupambana na ‘ Monkeypox ‘ katika majaribio appeared first on KITENGE BLOG.
By Author
Post a Comment