Mdogo wa Marehemu Augustino Lyatonga Mrema, Prof. Alex Mrema amesema wamekubaliana na wanafamilia wengine kuwa mazishi ya ndugu yao yatafanyika nyumbani kwao alipozaliwa, Kiraracha, Moshi mkoani Kilimanjaro siku ya Alhamisi, Agosti 25, 2022.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, nyumbani kwa marehemu Mrema, Prof. Alex Mrema amesema Kaka yake alikuwa anasumbuliwa na Pafu hali iliyopelekea, Agosti 15, 2022 afikishwe kwenye Hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa matibabu.
“Tumekubaliana wanafamilia wote tutasafirisha Jumatano na Alhamisi tutafanya ibada ya mazishi nyumbani Kiraracha, Moshi”, amesema Prof. Alex
Kwa upande wake, Mke wa Marehemu, Doreen Mrema amesema kuwa marehemu alikutwa na umauti akiwa mikononi mwake, amesema alikuwa Rafiki yake, Mwalimu wake na Mshauri wake katika maisha yao ya kila siku.
“Tunashukuru Mungu kwa maisha aliyoishi hapa duniani, tunashukuru Serikali kuungana na sisi katika msiba huu”, amesema Mke wa marehemu, Doreen Mrema.
Naye, Mtoto wa marehemu Mrema, Michael Mrema amesema siku ya Jumatano watafanya ibada ya kumuaga marehemu Baba yao katika Parokia ya Salasala jijini Dar es Salaam, Saa 7 mchana, Pia amesema baada ya Misa wataanza safari ya kuelekea Moshi, pia nyumbani hapo Kiraracha kutakuwa na Misa ya kuaga.
Baadhi ya viongozi mbalimbali wa Serikali na Wanasiasa wamemzungumzia marehemu Mrema kuwa alikuwa Mwanasiasa mzalendo aliyeipenda nchi yake ya Tanzania. Mrema amefariki duninia Jumapili, Agosti 21, 2022, saa 12:15 Asubuhi, katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam.
Mtoto wa Marehemu, Michael Mrema (Pichani)
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi (wa kulia) akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla msibani kwa Mzee Mrema, Salasala jijini Dar es Salaam.
By Mpekuzi
Post a Comment