Rais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kufuatia vifo vya watu 19 waliofariki katika ajali iliyotokea leo Shinyanga.
Watu 19 wamefariki na wengine 15 kujeruhiwa katika ajali hiyo iliyohusisha magari manne ikiwemo trekta Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga.
Katika rambirambi zake, Rais Samia amevitaka vyombo vya kusimamia usalama barabarani kuongeza umakini katika kudhibiti ajali hizo.
Ajali hiyo imetokea usiku wa August 08, katika Barabara ya Isaka kijiji cha Mwakata ambapo imehusisha gari dogo aina ya IST namba ya usajili T 880 DUE, Hiace T 350 BDX, Lori T 658 DUW pamoja na trekta.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni Kamanda wa Polisi Geita ACP. Henry Mwaibambe amethibitisha kutokea kwa ajali na kusema Dereva wa trekta amekimbia na juhudi za kumsaka zinaendelea.

The post Rais Samia atuma rambirambi za ajali ya Shinyanga appeared first on KITENGE BLOG.
By Author
Post a Comment