Njombe
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Njombe imefanya uchambuzi wa mfumo wa rushwa ya Ngono kwenye elimu katika halmashauri ya wilaya ya Ludewa na kubaini vitendo hivyo hususani katika upangaji wa vituo vya kazi.
Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Njombe Kassim Ephrem amesema katika kipindi cha mwezi April hadi Juni Mwaka huu,taasisi hiyo imefanya uchambuzi wa mifumo minne,ambapo katika halmashauri ya wilaya ya Ludewa kwenye mfumo wa rushwa ya Ngono ndani ya idara ya elimu ukibainika katika halmashauri hiyo.
Mkuu wa TAKUKURU amesema miongoni mwa hatua zilizochukuliwa na taasisi hiyo ni pamoja na kutoa maelekezo kwa viongozi wa sekta ya elimu kufanya ufuatiliaji kwa waalimu na upandishaji wa madaraja juu ya vitendo hivyo na kushirikiana na taasisi kudhibiti mianya ya rushwa kwa baadhi ya watendaji.
“Tumekaa na viongozi na kuwaomba wazingatie taratibu ya mifumo yao na kuhakikisha haitoi mianya ya vitendo vya rushwa kwa kile wanachokifanya na tutaendelea kufuatilia kwa ukaribu”Amesema Ephrem
Sambamba na hilo taasisi hiyo kwa kipindi cha mwezi April hadi Juni 2022 imefanikiwa kufanya ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo kumi na sita (16) yenye jumla ya thamani ya Tsh.6,598,622,861.04
Viongozi autoka taasisi hiyo Wakiwa katika picha ya patoja mara baada ya kutoa taarifa mwezi April hadi Juni Mwaka huu ya kazi zilizofanywa na taasisi hiyo
By Mpekuzi
Post a Comment