TEMDO ARUSHA WABUNI MTAMBO WAKUCHAKATA MAFUTA YA ALIZETI |Shamteeblog.


Na Pamela Mollel,Arusha

Taasisi ya Uhandisi na usanifu mitambo Tanzania (TEMDO)wabuni mtambo mpya wa kuchakata mafuta ya Alizeti yenye uwezo wakusafisha mafuta lita 1000 kwa siku

Akizungumza na vyombo vya habari katika maonesho ya nane nane jijini Arusha,Mkuu wa kitengo cha mawasiliano na masoko Dkt Sigisbert Mmasi alisema kuwa mtambo huo utakwenda kuwasaidia wajasiriamali kuboresha bidhaa zao ili kuendana na soko

Alisema kuwa mtambo huo wa kuchakata na kusafisha mafuta ya alizeti ni kivutio kikubwa katika maonyesho hayo huku akitaka wajasiriamali kuchangamkia fursa hiyo

"Awali kabla ya uwepo wa mashine hicho kulikuwepo na changamoto ya kusafisha mafuta hali iliyowalazimu wajasiriamali kuingia gharama kubwa kusafisha mafuta katika viwanda vikubwa"alisema Dkt Mmasi

Mbali na uwepo wa Teknolojia hiyo ya mashine ya kuchakata Alizeti pia TEMDO wana mashine mbalimbali ikiwemo ya kutengeneza siagi ya karanga,mashine ya kuchakata unga lishe na viungo vya kupigia,mashine ya kuchakata zao la muhogo na sukari Pia wanatengeneza vifaa tiba kama vile vitanda vya kujifungia wamama wajawazito.



 

By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post