WhatsApp sasa kuleft bila yoyote kujua |Shamteeblog.

Mtandao wa WhatsApp unatarajia kuzindua vipengele vipya kikiwemo cha kufanya watumiaji wao kuweza kuondoka kwenye magroup bila kila mtu kujua.

Katika kipengele hicho maAdmin pekee ndio watajua kama mtu ametoka kwenye kundi.

Mabadiliko hayo yatawezesha pia watu kuamua nani awaone wakiwa “online” na kuzuia “screenshots” za meseji zinazoruhusiwa kufunguliwa mara moja tu.

Mkurugenzi Mkuu wa Meta,Mark Zuckerberg ameeleza kuwa vipengele hivyo vitaanzia Uingereza na India.

“Tutaendelea kujenga njia mpya za kulinda jumbe zenu ili ziwe kama mazungumzo ya uso kwa uso.”

The post WhatsApp sasa kuleft bila yoyote kujua appeared first on KITENGE BLOG.



By Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post