Maafisa watano wa halmashauri ya wilaya ya Mbulu mkoani Manyara wamesimamishwa kazi kwa matumizi mabaya ya madaraka.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Innocent Bashungwa amesema watu wamewekwa pembeni ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili.
Maafisa hao ni kaimu mkuu wa kitengo cha manunuzi Juma Mavumo, aliyekuwa kaimu mweka hazina Ramadhani Mwakamyanda, Mweka hazina wa sasa Respicius Kagaruki, mkuu wa kitengo cha TEHAMA Nyanda Msirikale na mhasibu wa mapato David Assey.
Julai 12 mwaka huu aliyekuwa anakaimu ofisi ya Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya Mbulu, David Assey anadaiwa kuandika barua kwa kampuni binafsi na kukopa shilingi milioni 6.7 kwa aijli ya matumizi ya ofisi na kuelekeza fedha hiyo kuwekwa kwenye akaunti yake binafsi.
The post 5 wasimamishwa kazi kwa matumizi mabaya appeared first on KITENGE BLOG.
By Author
Post a Comment