Na Jeremiah Sulle
UEFA Nations League ni maashindano ya soka la kimataifa yanayofanyika kila baada ya miaka miwili yakishirikisha timu za taifa za nchi 55 wanachama wa Shirikisho la soka la Ulaya (UEFA).
Dhumuni la kuanzishwa kwa mashindano haya ni kuwapa wachezaji mechi za kiushundani badala ya mechi za kirafiki zisizo na ushindani mkubwa.
Kwa kifupi michuano hii inachukua nafasi ya mechi za kirafiki zisizo na ushindani mkubwa kwa mfano kuepusha Mataifa kama Uhispania na Ufaransa kukutanishwa na Mataifa kama San Marino na Moldova.
Muundo wa Ligi ya Mataifa ya Ulaya
Mfumo wa mashindano ya UEFA Nations League umegawanyika katika makundi manne yanayoitwa Ligi (leagues) A , B, C, na D.
Ligi A, B na C zimeundwa na timu 16 huku Ligi D ikiundwa na timu 7.
Ligi A,B na C zimegawanyika katika makundi manne kila mmoja huku Ligi D ikigawanyika katika makundi mawili huku kundi moja likiwa na timu 4 na kundi lingine likiwa na timu 3.
Upangaji wa timu kwenye Ligi husika unafayika kulingana na mfumo wa viwango vya uwiano wa UEFA na nafasi ya nchi husika kwenye mashindano yaliyopita.
Washindi wanne wa makundi ya Ligi A huingia katika raundi ya mwisho ili kumpata bingwa wa Nations League. Hizi ni mechi za mtoano za mchezo mmoja unaochezwa katika uwanja usiofungana na upande wowote.
Washindi wa Kundi kutoka ligi zingine hupandishwa daraja hadi Ligi A huku Mataifa ambayo yanamaliza nafasi ya pili na ya tatu katika kundi lao husalia kwenye Ligi husika kwa mashindano yajayo.
Mataifa yanayomaliza nafasi ya nne katika Ligi A na B hushuka daraja jambo ambalo limeikuta ENGLAND jana baada ya kipigo cha 1-0 dhidi ya Italia na kushuka kwenda Ligi B.
We you are gb
The post Ifahamu michuano ya ‘UEFA Nations League’ appeared first on KITENGE BLOG.
By Author
Post a Comment