Kaka yake na mshambuliaji wa Juventus Paul Pogba, aitwaye Mathias ( kulia katika picha) pamoja na washikaji zake wameshitakiwa kwa kosa la kutaka kunyang’anya pesa za mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United.
Mathias
Pamoja na washikaji zake wanne wapo chini ya ulinzi kwa sababu ya uporaji na kujihusisha na genge la wahuni.
Hata hivyo, mwanasheria wa Mathias Yassine Bouzrou amesema mteja wake ni mtu asiye na makosa.
Ameviambia vyombo vya habari vya Ufaransa kuwa jambo hilo watalipinga kwa nguvu zote.
Pogba, ambaye pi ni mchezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa amesema kuwa hivi karibuni alipokea vitisho kutoka kwa genge la wahuni wakitaka kumpora kiasi cha paundi milioni 11.29.
Na kaka yake Mathias kupitia video inayosambaa amekiri ni kweli alikuwa sehemu ya mpango huo.
Mathias pia ni mchezaji mpira wa kulipwa na amechezea vilabu kadhaa barani Ulaya.
The post Kaka wa Pogba ashitakiwa kutaka kupora fedha za mdogo wake appeared first on KITENGE BLOG.
By Author
Post a Comment