Mabaki ya mwili wa mwanafunzi, Levis Mwailemale (16) wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Ikuti iliyoko wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya, aliyepotea zaidi ya miezi nane iliyopita yamekutwa porini pamoja na nguo alizokuwa amevaa wakati anapotea.
Familia imeeleza kuwa kijana Levis Mwailemale alipotea katika mazingira ya kutatanisha Januari 9 mwaka huu, ambapo walianza jitihada za kumtafuta bila mafanikio hadi Septemba 18 walipokuta mabaki ya mwili wake.
Hata hivyo maziko ya mwili wa kijana huyo yalifanyika baada ya Jeshi la Polisi kukamilisha uchunguzi wake na kutoa kibali.
EATV
from Author
Post a Comment