MMOMONYOKO WA MAADILI NDANI YA JAMII WACHANGIA UNYANYASAJI KIJINSIA. |Shamteeblog.



Na John Walter-Dar es Salaam.

Kuvunjika kwa maadili katika familia na jamii kwa ujumla ni mojawapo ya sababu zinazotajwa kuchangia kwa viwango vikubwa kutokea kwa wimbi la vitendo vya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji hapa nchini.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikisha waraghibishi ngazi ya vijiji kutoka kata tatu za Rubeho wilaya ya Gairo mkoa wa Morogoro, Mamire wilaya ya Babati mkoa wa Manyara na Vumari wilaya ya Same mkoa wa Kilimanjaro imetajwa kuwa na viwango vya juu vya mmomonyoko wa maadili.

Akiwasilisha mrejesho wa awali wa matokeo ya utafiti huo katika mafunzo ya uongozi ngazi ya jamii kwa waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, Afisa Mwandamizi Tathimini na Ufuatiliaji kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Sylivester Mavanza alisema kuporomoka kwa maadili miongoni mwa wakazi wa kata hizo imeleta athari zinazochangia kutokea kwa viwango vikubwa vya wimbi la vitendo vya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji.

Mavanza alisema utafiti huo umefanikiwa baada ya waraghibishi kupewa mafunzo maalumu ya kuibua changamoto zinazotokana na ukatilia wa kijinsia katika maeneo yao ambapo walibaini kuwepo kwa ukatili wa kingono ngazi ya familia huku wakieleza vitendo hivyo vimekithiri kutokana na kuporomoka kwa maadili.

“Mojawapo ya mambo tuliyoyabaini wakati wa utafiti wetu ni pamoja na usambazaji wa picha za ngono kupitia mitandao ya kijamii ikiwepo makundi ya Whatsap, lakini kikubwa zaidi Kata ya Rubeho inaongoza kwa vitendo vya ubakaji wa Mtungo ikilinganishwa na kata nyingine za Mamire Wilaya ya Babati na Vumale Wilaya ya Same”. Alifafanua Bw. Mavanza.

Alitaja vitendo vingine kuwa ni ubakaji, ulawiti kucheza ngoma za ngono, kufanya mapenzi bila kinga, manyanyaso kwenye jamii na muziki wa vigodoro ambavyo kwa pamoja vimekuwa chanzo cha Mimba za utotoni na matumizi ya dawa za kulevya hususani bangi.

Mraghibishi kutoka (TGNP Bi Asteria Kantuzi) alisema kwa upande wa kata ya Vumari Wilayani Same Mkoani Kilimanajro ulegevu wa wazazi katika malezi ya kusababisha vijana wengi kutumbukia katika vitendo viovu ikiwemo matumizi y miadarati,wizi na mahusiano ya kimapenzi kati ya ndugu kwa ndugu.

“Wazazi na jamii wameshindwa kuchukua hatua kwa watoto hatimae wamejiingiza kwenye vitendo vya matumizi ya mirungi na bangi na kupelekea mmomonyoko wa maadili.”alisema Asteria.

Kwa upande wake, Mratibu wa Mradi wa Wanawake Vijijini Kuleta Mabadiliko kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi Catherine Kasimbasi alietembelea kata ya Mamire wilaya ya Babati mkoa wa Manyara alisema changamoto kubwa iliyopo eneo hilo ni Ukeketaji kwa watoto wachanga, lugha za udhalilishaji, ubakaji na ulawiti.

“Ili kukabiliana na chanagamoto hizo, Mtandao wa jinsia Tanzania TGNP umeunda vikundi raghibishi katika maeneo hayo ili kutoa elimu itakayosaidia jamii hiyo kuacha vitendo hivyo vya ukatili.”


 

By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post