Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi, Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa Cde. Victoria Mwanziva amewapongeza vijana ambao wameshiriki mchakato wa Uchaguzi ndani ya Chama kupitia Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa chama hicho.
Mwanziva ametoa pongezi hizo kwa uthubutu wao, Ushiriki wao akisema ni alama kubwa kwa maisha yao ya uongozi na Jumuiya kwa ujumla.
Ameongeza kuwa kujitokeza kwao na kugombea kwa wingi imedhihirishia ni kwa kiasi gani hamasa imekuwa kubwa katika Chaguzi za Umuja wa Vijana(UVCCM)
"Mliopata nafasi na kushinda nawapongeza kwa kuaminiwa na vijana. Mmepewa Imani, walipeni utumishi uliotukuka. Nawasihi, usiruhusu cheo kikakubadirisha ukadharau wengine, ukajiona bora, mwenye haki, weledi, upeo na uwezo kuliko wengine ambao hawakupata nafasi au unaowaongoza"
Amesema Mwanziva
Aidha, amewakumbusha kwenda kusimamia utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020-2025 katika Wilaya zao. Amewakumbusha kuzingatia miiko na Katiba ya CCM na kushirikiana na wagombea walioshindana nao maana wana wanazo ajenda nzuri pia wakizileta pamoja watapiga hatua kubwa.
"Viongozi na Wenyeviti wapya wa UVCCM ngazi ya Wilaya mlioaminiwa nendeni mkatekeleze majukumu yenu kwa kuzingatia Kanuni za UVCCM na Katiba ya CCM. Nendeni mkawe chachu na madaraja ya Mapinduzi ya Maendeleo katika Wilaya zenu" Amesisitiza Mwanziva
Mwisho ametoa rai kwa vijana kuendelea kujitokeza na kushiriki chaguzi mbalimbali na kuwa mstari wa mbele kwa kufuatilia na kushiriki masuala ya kitaifa na kujihusisha na mustakabali wa uongozi wa nchi yao.
By Mpekuzi
Post a Comment