Mafuriko yameikumba Australia na kuharibu miundombinu ya barabara na kupelekea shule kufungwa.
Madhara mengine ni pamoja na umeme kukatika huku nyumba 3,000 zikiharibiwa.
Waziri Mkuu Daniel Andrews amesema kuna uwezekano idadi ya wahanga wa mafuriko ikaongezeka.
Amesema nchi hiyo imekutwa na mafuriko ambayo hayajawahi kutokea kwa miaka mingi.
” Nadhani huenda tukawa na hali hii kwa muda ,” amesema Waziri Mkuu huyo kuliambia Shirika la Habari la nchi hiyo.
Mmoja wa wahanga ni Barry Webster ambaye nyumba yake imezama katika maji.
” Siku zote nilitamani kuwa karibu na mto au maji, lakini sio kwa nilichokiona,” amesema mhanga huyo.
Kwa mujibu wa mamlaka za nchi hiyo, mvua zimenyesha kupita kiwango cha kawaida na kuleta madhara makubwa.
Katika baadhi ya miji. watu wametakiwa kuhama ili kuepuka madhara zaidi.
Mafuriko hayo yamesababishwa na athari za Mabadiliko ya Tabia ya Nchi.
The post Australia yakumbwa na mafuriko appeared first on KITENGE BLOG.
By Author
Post a Comment