CCM YAWAONYA WANAOTENGENEZA 'MIUNDOMBINU HARAMU' KUKWAMISHA VIONGOZI BORA |Shamteeblog.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo ameonya baadhi ya wanachama wanaotengeneza kitu alichokiita ni ‘miundombinu’ haramu, inayohusisha vitendo vya rushwa, fitna na majungu ili kuwadhibiti watu bora wenye sifa nzuri za kuchaguliwa kuwa viongozi wasipate nafasi ya kushika dhamana za uongozi ndani ya chama.

Aidha pamoja na onyo hilo Ndugu Chongolo pia amesisitiza kuwa CCM iko makini na inafuatilia kwa karibu mchakato wote wa uchaguzi katika ngazi zote za muundo wa chama, ambao sasa umefikia ngazi za mikoa, ili kudhibiti vitendo vyote vya ukiukwaji wa taratibu, vikiwemo vitendo vya rushwa, akionya kuwa chama hakitasita kuchukua hatua kali, kama kilivyofanya kwenye ngazi ya wilaya, ambapo baadhi ya chaguzi zimerudiwa, baada ya kufutwa.

Katibu Mkuu Chongolo ameyasema hayo leo Jumamosi Oktoba 22, 2022, Kigamboni, jijini Dar es Salaam, baada ya kuweka jiwe la msingi katika Ofisi ya CCM Wilaya ya Kigamboni pamoja na kukagua mradi wa ujenzi wa nyumba ya makazi ya Katibu wa Chama Mkoa wa Dar es Salaam, unaoendelea katika eneo la Somangila, Kigamboni.

"Chama hiki kina watu na wanachama wenye sifa nzuri kabisa za kuwa viongozi bora, wenye mioyo safi, wana ari kubwa ya kuwatumikia wananchi na wanachama, chama hiki kina watu wenye kila aina ya ujuzi na uwezo, lakini changamoto yetu ni baadhi ya wanachama kutengeneza miundombinu haramu ya kuwadhibiti watu wazuri wasipate dhamana za uongozi na waweke watu dhaifu kwa maslahi yao, hili chama tupo macho na tunafuatilia kwa karibu," amesisitiza Katibu Mkuu.

Aidha, Katibu Mkuu amewataka watendaji wa chama katika ngazi zote, kusimamia taratibu na kuweka mipango imara kuhakikisha mali na rasilimali za chama zinalindwa na kuziba mianya yote inayoweza kusababisha upotevu wake.

"Inasikitisha kuona mali ambazo chama inazimiliki kwa muda mrefu leo baadhi ya watu wanasubiri kuona zikipokonywa, tena wengine wanajitengenezea na uhalali… ili wazipore. Chama kitawachukulia hatua watendaji wote ambao watashindwa kusimamia na kulinda mali za chama hiki au kuacha tu zikipokonywa," amesema Katibu Mkuu Ndugu Chongolo.

Katika hatua nyingine Katibu Mkuu amewapongeza wanachama wote waliotumia haki yao ya kugombea na kuchaguliwa kushika nafasi mbalimbali za uongozi na amewataka kuhakikisha wanazitumikia kikamilifu dhamana hizo, akiwataka watambue kuwa, kuaminiwa kwao ni ishara ya kubeba wajibu wa kuzidi kukijenga na kukiimarisha chama chao.

"Mmepewa dhamana ya kuongoza kwa kipindi cha miaka mitano, nendeni mkasimamie Ilani pamoja na miradi ya maendeleo kwa tija na kuhakikisha thamani ya fedha, hii itakisaidia chama kujiweka katika mazingira mazuri katika uchaguzi wa mwaka 2024 na 2025. Tuliomba dhamana ya kuongoza nchi. Tukisimamia vizuri Ilani ya Chama Cha Mapinduzi na kutatua changamoto za wananchi, hatutakuwa na maswali mwaka 2024 na 2025 bali tutakuwa na majibu.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akizungumza jambo kwenye hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba ya Katibu wa CCM mkoa wa Dar Es Salaam pamoja na Ofisi ya chama hicho Wilaya leo Oktoba 22,2022.PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-KIGAMBONI


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akikata utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Ofisi ya CCM wilaya iliopo katika kata ya Somangira Wilaya ya Kigamboni,ambapo pia ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba ya Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam.

Pichani juu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akiwaaongoza viongozi wa chama hicho mkoa kufunua kitambaa kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Ofisi ya CCM wilaya iliopo katika kata ya Somangira Wilaya ya Kigamboni,leo Oktoba 23,2022 jijini Dar es Salaam.

Muonekano wa nje wa Ofisi ya CCM wilaya ya Kigamboni iliyowekwa jiwe la Msingi la Ujenzi na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo leo Oktoba 22,2022 Kigambon jijin Dar.
PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-KIGAMBONI



Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akiongoza Viongozi wengine wa CCM mkoa wa Dar Es Salaam wakati kukata utepe wakati wa hafla ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba ya Katibu wa CCM mkoa wa Dar Es Salaam.

Burudani ilikuwepo kutoka kwa Kundi la Makilikili wa Kigamboni

Baadhi ya Viongozi wa CCM wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri.
PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-KIGAMBONI

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akimsikilia Mbunge wa Jimbo la Kigamboni Mhe.Faustine Ndugulile alipokuwa akizungumza mbele ya wanachama mbalimbali wa chama hicho waliofika kwenye hafla hiyo.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo akisalimiana na viomgozi mbalimbali mara baada ya kupokewa kwa ajili ya kushiriki hafla fupi ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi ofisi ya CCM wilaya ya Kigamboni na Nyumba ya Katibu Mkuu wa CCM mkoa leo Oktoba 22,2023 jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Kigamboni Mhe.Faustine Ndugulile

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akipita mbele ya Vijana wa Chipukizi alipowasili Somangira kwenye hafla ya kuweka jiwe la msingi wa ujenzi wa ofisi ya CCM Wilaya ya Kigamboni leo Oktoba 22,2022.
PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-KIGAMBONI



Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akiwa ameongozana na viongozi wa chama hicho Wilaya ya Kigamboni na Mkoa akielekea kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Ofisi ya CCM wilaya iliopo katika kata ya Somangira Wilaya ya Kigamboni mkoani Dar es Salaam leo Oktoba 22,2022
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akipwea maelezo kuhusu jengo la ofisi hiyo (haipo pichani) alipofika kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Ofisi hiyo iliopo katika kata ya Somangira Wilaya ya Kigamboni mkoani Dar es Salaam leo Oktoba 22,2022
.PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-KIGAMBONI



Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akiwa kwenye picha ya pamoja na Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuwela jiwe la msingi wa nyumba ya Katibu wa CCM mkoa wa Dar Es Salaam.



By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post