Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini, bei hizi zitaanza kutumika kuanzia Jumatano, tarehe 5 Oktoba 2022 saa 6:01 usiku.
“Bei za Mafuta yaliyosafishwa katika soko la dunia kwa mwezi Agosti 2022 ambazo zimetumika katika kukokotoa bei za mafuta za hapa nchini katika mwezi wa Oktoba 2022 zimepungua kwa asilimia 7.4, 3.9 and 1.9 kwa mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa, mtawalia, ikilinganishwa na bei hizo kwa mwezi Julai 2022”
“Hata hivyo, ikilinganishwa na gharama za uagizaji zilizotumika katika kukokotoa bei za Septemba 2022, gharama za uagizaji wa mafuta zimeongezeka kwa kati ya asilimia 50 na 163 kwa kutegemea bandari na bidhaa husika ikilinganishwa na gharama za uagizaji zilizotumika katika kukokotoa bei za Septemba 2022, na hivyo kuathiri mwenendo wa bei za mafuta hapa nchini”
“Pamoja na hayo, kufuatia dhamira ya Serikali ya kuendelea kupunguza madhara ya ongezeko la bei za mafuta hapa nchini kwa wananchi na uchumi kwa ujumla, Serikali imetoa ruzuku ya shilingi bilioni 59.58 kwa ajili ya bei za mafuta ya Oktoba 2022 “
TAZAMA HAPA CHINI
By Mpekuzi
Post a Comment