Kampuni ya uuzaji na unganishaji wa magari na mitambo ya Gf Trucks & Equipment’s Ltd imeibuka kuwa kampuni ya kwanza inayouza na kusambaza Magari na mitambo ukanda wa mikoa ya kanda ya ziwa.
Hayo yamejiidhihirisha wakati wa kufunga maonesho ya 5 ya teknolojia ya madini mkoani Geita na kuibuka kampuni bora ya usambazaji na uuzaji wa mitambo.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo na Waziri wa Viwanda na uwekezaji Ashatu Kijaji,Afisa masoko na mauzo wa kampuni ya GF Poul Msuku alisema wanafurahia kuibuka washindi katika kipengele hicho na wanachukua tuzo hiyo kama chachu ya kujipanga na kuongeza nguvu kaitia uwekezaji kwa kanda ya ziwa.
Gf Trucks ambao ni wauzaji wa mitambo na mashine za migodini aina ya XCMG, na magari ya kubebea mizigo ya FAW na Hongyang wana wateja wengi wanaojihusisha na Uchimbaji wa madini na shughuli za usafirishaji nchini,
Pia Gf waliitumia siku ya kufunga maonesho kwa kukabidhi Mtambo wa kuchimbia madini kwa mteja aliyenunua katika maonesho hayo ya madini kwa bei ya punguzo.
Pia Waziri Kijaji aliwataka Gf kuwekeza zaidi katika kwawezesha wachimbaji wadogowadogo ili waweze kujikomboa na kwa kuwawekea utaratibu rahisi kumudu gharama, ikiwemo mikopo rahisi na pia aliwataka wachimbaji hao kuchapa kazi itakayoweza kumwongezea kipato na kulipa kodi kwa maendeleo ya nchi.
Nae Mkuurugenzi wa kampuni ya G Unity Squre Ltd,Ezekiel Rembo aliwashukuru GF kwani kwa kushiriki katika maonesho hayo, wameweza kununua mashine hiyo (XCMG) kwa gharama nafuu tofauti kama wangeifuata Dar essalaam na kwamba ameokoa zaidi ya shilling million 10 ikiwamo gharama ya mafuta kuitoa Dar hadi Geita alimaliza .
Waziri wa viwanda na uwekezaji Ashatu Kijaji akimkabidhi funguo ya mtambo wa kuchimbia Madini (Excavator ) ya XCMG Mkurugenzi wa kampuni ya G Unity ,Ezekiel Rembo baada ya kununua katika maonyesho ya madini kwa punguzo malum mkoani Geita
Mkurugenzi wa E Unity akiangalia mtambo wa Excavator baada ya kukabidhiwa katika viwanja vya maonyesho
By Mpekuzi
Post a Comment