Na Khadija Kalili, Kibaha
NAIBU Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete amewapongeza Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) kwa huduma wanayoendelea kuitoa ya usajili kwenye Maonesho ya tatu ya Uwekezaji na Bashara yanayoendela kweye viwanja vya Stendi ya Zamani Mailimoja Kibaha Mkoani Pwani.
Mheshimiwa Kikwete alisema hayo jana Oktoba 9 alipotembelea kwenye banda la BRELA na kufanikiwa kumkabidhi kijana Idriss Njeru cheti chake cha usajili.
"Lazima vijana mjifunze kufanya kazi kwa kufuata kanuni na taratibu za serikali kama jinsi wewe ulivyojisajili nakupongeza sana"amesema Mheshimiwa Kikwete.
Ameongeza kwa kusema kuwa vijana lazima mjisajili hasa kwa Kampuni za Teknolojia kwani ukijisajili unakuwa vizuri na unakuwa na ulinzi katika utendaji wa kazi zako".
Endeleeni kufanya kazi kwa njia halali na kuingia katika mfumo rasmi wa serikali,hongera sana kwa kupata usajili kwani hii ni sehemu ya kuchangia pato la taifa "amesema Kikwete.
Nenda ukawe balozi mzuri kwa vijana wenzako kua mjanja ni pamoja na kujisajili BRELA huku ukifanya kazi nzuri zenye kuzingatia maadili ya Mtanzania kwani kuna mambo mengi ya kuisadia jamii yanayopaswa kufanywa huku ukiwa ndani ya mfumo uliosajiliwa rasmi.
Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete akimkabidhi cheti cha usajili BRELA Idriss Njeru anaye shuhudia ni Afisa Msajili Francis Filimbi
Baadhi ya wananchi wakifuatilia jambo kwenye banda la BRELA.
By Mpekuzi
Post a Comment