Uwenda kwenye macho ya wengine ikawa sio hatua kubwa sana ya kimuziki, waliopiga Cheed na Killy wakiwa Kings Music, lakini hakuna jambo gumu kama kumfanya mtu aonekane/ajulikane kwa watu na kuzingatiwa. Cheed na Killy ni wasanii ambao wamejulikana na wengi kupitia mgongo wa Kings Music, Ukiachana na Nyimbo zao kama kundi, lakini hata solo projects zao zilisikika zaidi masikioni mwa watu.
Kwa ukubwa wa Harmonize kwenye muziki, wengi tuliamini angekuwa kiunganishi kizuri cha kuwatoa wasanii hawa pale walipoishia, Kings Music na kuwafikisha sehemu nyingine kubwa, ila bahati mbaya sana haijawa hivyo, angalau kwa Killy kuna mwanga kwake ulionekana, kuna mawe aliachia ila yakakosa promo ya uhakika, sawa kwa Cheed ambaye hakutengeneza ngoma kali sana akiwa Konde, ila bado hata kwa hizo kali za kawaida, zikapewa mgongo.
Bila kuivunjia heshima label yoyote nchini, Kwenye suala la Record Label, lazima tuwaheshimu sana WCB, strategies zao kwa wasanii wao ni za hali ya juu sana, wanamchukua msanii toka point 0 hadi point 1 na kuendelea, Kwa Konde Gang imewachukua Cheed na Killy toka point +1 hadi point -1. Hii haimaanishi hakuna upande ambao Konde Gang imefanikiwa, Ibrah na Anjella ni kielelezo kizuri cha mafanikio ya Label hiyo.
Kiufupi usainishwaji wa Cheed na Killy pale Konde Gang ulikuwa ni wa mihemko, Ni muda sasa wa Harmonize kuwa na vision ya Label yake sio kujiendea tu. Cheed na Killy walikuwa na mafanikio makubwa zaidi Kings kuliko Konde Gang.
from Author
Post a Comment