Korea Kusini imeipatia Tanzania mkopo wa gharama nafuu wa shilingi bilioni 310 kwa ajili ya upanuzi wa mfumo wa utambuzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Mkopo huo pia ni kwa ajili ya uendelezaji na utunzaji wa mfumo wa taarifa za ardhi.
Hafla ya utiaji saini wa mikataba hiyo imefanyika nchini Korea mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Mkataba wa awamu ya pili ya mradi wa upanuzi wa mfumo wa utambuzi wa NIDA una thamani ya shilingi bilioni 161 na mkataba wa uendelezaji na utunzaji wa mfumo wa taarifa za ardhi ambao una thamani ya shilingi bilioni 149.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa Tanzania na Korea zinajivunia mahusiano yaliyodumu kwa miaka 30 ambayo yamekuwa chachu katika kukuza uchumi wa nchi hizo mbili katika sekta mbalimbali.
The post Korea yaipatia TZ mkopo wa bilioni 310 appeared first on KITENGE BLOG.
By Author
Post a Comment