Moto mwingine umezuka katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha mkoani Iringa, ikiwa ni siku chache baada ya moto kuunguza hifadhi ya mlima Kilimanjaro.
Habari kutoka mkoani Iringa zinasema moto huo umeunguza sehemu ya hifadhi hiyo.
Hata hivyo, Mkuu wa hifadhi hiyo, Kamishna Msaidizi wa Uhufadhi, Godwell Meing’ataki amesema juhudi za kuuzima moto huo zinaendelea.
Meing’ataki amesema kuwa moto huo umesababishwa na majangili wanaorina asali katika hifadhi hiyo.
Amesema maofisa wa hifadhi na wananchi wameshirikiana kuukabili moto huo.
The post Moto wazuka hifadhi ya Ruaha appeared first on KITENGE BLOG.
By Author
Post a Comment