Mwakyembe kuchunguza sababu ya kufeli Shule ya Sheria |Shamteeblog.

Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Damas Ndumbaro amemteua Dk Harrison Mwakyembe kuongoza kamati ya watu 7 itakayochunguza chanzo cha wanafunzi wanaosoma mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo (LST) kufeli kwa wingi katika mitihani yao.

Mwakyembe aliwahi kushika nafasi mbalimbali za Uwaziri katika serikali.

Kuundwa kwa kamati hiyo kunafuatia taarifa ya kushtusha iliyoripotiwa juu ya wanafunzi wengi kufeli mitihani yao.

Katika kamati hiyo, Daktari Ndumbaro pia amemteua mshauri wa zamani wa Rais mstaafu Jakaya Kikwete Cililius Matupa ambaye ni kwa sasa ni Jaji mstaafu.

Pia yumo Rashid Asaa ambaye ni Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma wa Zanzibar.

Wengine ni Gloria Kalabamu, Makamu wa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika, Alice Mtulo, Wakili mwandamizi kutoka Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Mary Mniwasa, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Dar Stock Exchange na John Kaombwe ambaye ni Mwanafunzi aliyehitimu LST.

Kamati hiyo itakabidhiwa hadidu rejea na Kàtibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mary Makondo kesho Oktoba 13, 2022 na itafanya kazi kwa siku 30.

Katika miaka ya nyuma, shule hiyo ilikuwa ikifaulisha kwa kiwango cha wastani wa asilimia 81

The post Mwakyembe kuchunguza sababu ya kufeli Shule ya Sheria appeared first on KITENGE BLOG.



By Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post