Rais Samia: Vijana wanahangaika na supu ya Pweza, vumbi la Kongo |Shamteeblog.

Rais Samia Suluhu Hassan ameagiza kufanyika utafiti wa kwanini vijana balehe wanakuwa na lishe ndogo wakati taifa linahitaji vijana wenye nguvu kwa maendeleo ya taifa.

Akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba wa usimamiaji shughuli za lishe, Rais Samia amesema kuna haja ya kufanyika kwa tafiti hiyo ili kuja na majibu na kuyatafutia ufumbuzi.

“Watoto balehe lakini unakuta wana afya duni,au ndio fasheni, wengine wanataka kuwa slim,” amesema.

Amesema wakati wakutafuta watoto vijana hao wanahangaika mara kunywa supu ya pweza na kwamba kuna tatizo ambalo wanalijua lakini wanalificha.

“Watafiti fanyeni tafiti, inaonekana kuna tatizo linawaumiza watoto wetu,” amesema.

“Mara wengine wanahangaika na vumbi la Kongo, mara kitu gani lakini tatizo kubwa liko kwenye lishe,” amesema.

Amesema kuendelea kwa hali hii kunapelekea kuwa na taifa goigoi wakati taifa linategemea rasilimali watu na nguvu kazi.

The post Rais Samia: Vijana wanahangaika na supu ya Pweza, vumbi la Kongo appeared first on KITENGE BLOG.



By Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post