Serikali imesema itafanya jitihada uhamasishaji wa usomaji wa vitabu nchini. |Shamteeblog.


Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof.  James Mdoe wakati akifunga tamasha la 31 la vitabu lililomalizika jana tarehe 15/10/2022  katika viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar es salaam. 

Amesema kuwa sasa ni wakati wa kuendeleza ushirikiano na sekta binafsi ambao ni waandishi na wachapishaji katika kuhakikisha wanarejesha ari ya usomaji wa vitabu nchini.

"Kwa kweli niwapongeze kwa jitahada za kuhakikisha tamasha hili linafanyika japo kuwa kuna mapungufu ambayo kwa ushirikiano tutaweza kuyatatua katika matamasha mengine yajayo"amesema Prof.Mdoe.

Prof.Mdoe amesema kuwa Utamaduni wa usomaji nchini umeshuka kwa kiasi kikubwa  hivyo lazima kuwe na mbinu za kuhakikisha unarejea kama ilivyo kawaida. 

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) ,Mkurugenzi wa  Idara ya Utafiti ,Habari na Machapisho Bwana.Kwangu Masalu ameshukuru uongozi wa PATA kuweza kuwashirikisha katika maonesho haya .

Amesema wataendelea kufanya kazi kwa karibu na PATA katika kuhakikisha kazi ya uandishi na uchapishaji inafanyika vizuri kwa weledi.

Maonesho yajayo yatakuwa makubwa ambayo yatasaidia katika uhamasishaji wa usomaji wa vitabu nchini na watanzania kupata fursa ya kusoma machapisho mbalimbali kutoka kwa wachapishaji binafsi.










By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post