Taasisi ya Endeleza Wazee Kigoma yazindua harambee ya kitaifa ya ujenzi wa kituo |Shamteeblog.

Taasisi ya Endeleza Wazee Kigoma imezindua harambee ya kitaifa ya ujenzi wa kituo cha mfano cha kutoa huduma za afya, burudani na ustawi wa wazee.

Kituo hiko cha mfano kinatarajiwa kuleta mabadiliko, fikra na mtazamo juu ya wazee katika jamii na nchi kwa ujumla. Kauli mbiu ya harambee hiyo ni "Jana nilikuwa kijana kama wewe,  kesho utakuwa mzee kama mimi, nichangie nipumzike”.

Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika jana jijini Dar es salaam, Mgeni Rasmi katika Harambee hiyo Balozi Mama Getrude Mongela alisema Watanzania wanatakiwa kuwajali na kuwatunza wazee, na pia waungemkono juhudi za Taasisi ya Endeleza Wazee Kigoma kwenye kujenga kituo cha wazee Kigoma.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Endeleza Wazee Kigoma, Mama Clotilda Kokupima amesema kwa upande wao wamejipanga katika kusaidia wazee na kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuboresha huduma kwa wazee nchini.
Balozi Mama Getrude Mongela akizungumza katika hafla ya kitaifa ya kuchangia ujenzi wa kituo cha mfano cha kutoa huduma za afya, burudani na ustawi wa wazee, iliyofanywa na Taasisi ya Endeleza Wazee Kigoma (EWAKI), katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam jana. Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Endeleza Wazee Kigoma, Mama Clotilda Kokupima 


 



By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post