TANZANIA NA DRC ZASAINI HATI YA MAKUBALIANO (MOU) |Shamteeblog.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 23 Oktoba, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 23 Oktoba, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya mazungumzo yake na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 23 Oktoba, 2022.

 Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo, akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya mazungumzo yake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 23 Oktoba, 2022.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo wakati wakishuhudia uwekaji saini Mkataba wa makubaliano baina ya Tanzania na DRC, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 23 Oktoba, 2022. Kwa upande wa Tanzania, Mkataba huo ulisainiwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye na kwa upande wa DRC uliwekwa saini na  Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya nje wa DRC, Mhe. Christophe Lutundula.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal 2 Jijini Dar es Salaam tarehe 23 Oktoba, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo wakati wa Wimbo wa Taifa wa Tanzania ukipigwa mara baada ya Rais huyo wa DRC kuwasili nchini tarehe 23 Oktoba, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo wakati wakiangalia vikundi mbalimbali vya ngoma za asili vikitumbuiza mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal 2 Jijini Dar es Salaam tarehe 23 Oktoba, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo akikagua Gwaride la Heshima lililoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal 2 Jijini Dar es Salaam tarehe 23 Oktoba, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal 2 Jijini Dar es Salaam tarehe 23 Oktoba, 2022.



By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post