CHAMA cha Wanawake Wafanyabiashara (TWCC) kimeandaa ziara ya wafanyabiashara 50 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzani kuelekea katika ziara ya kibiashara nchini Uturuki Oktoba 11 - 19, 2022.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 11, 2022 jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake Wafanyabiashara (TWCC) Taifa Mrs. Mercy Sila amesema wafanyabiashara hao ni kutoka mikoa ya Tabora, Mbeya, Dar es Salaam, Mwanza, Kigoma, Morogoro, Mtwara, Simiyu.
Amesema kuwa ziara hiyo imeandaliwa na Chama cha Wanawake Wafanyabiashara wa TWCC na Wafanyabiashara nchini Uturuki ili wafanyabiashara kujenga mtandao wa kibiashara baina yao na wafanyabiashara nchini Uturuki kupitia mikutano ya ana kwa ana (B2B), pia watatembelea maonesho makubwa ya kibiashara, kujifunza teknolojia mbalimbali, na kutembelea viwanda vya uzalishaji.
Ziara hiyo itaanza 11 hadi 19 Oktoba 2022, katika mji wa Istanbul uliopo nchini Uturuki.
Mwenyekiti wa TWCC Taifa Mrs. Mercy Sila na akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Oktoba 10, 2022 kuhusu Ziara ya Wafanyabiashara nchini Uturuki itakayofanyika kuanzia tarehe 11 - 19 Oktoba 2022.
Mfanyabiashara kutoka Mbeya, Bi. muliroseinez ni akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Oktoba 10, 2022 kuhusu Ziara ya Wafanyabiashara nchini Uturuki itakayofanyika kuanzia tarehe 11 - 19 Oktoba 2022.
Mkurugenzi Mtendaji wa TWCC Bi. mwajuma_hamza akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Oktoba 10, 2022 kuhusu Ziara ya Wafanyabiashara nchini Uturuki itakayofanyika kuanzia tarehe 11 - 19 Oktoba 2022.
By Mpekuzi
Post a Comment