UJENZI WA BARABARA YA MATOMONDO-MLALE JKT WAFIKIA ASILIMIA 65,MKUU WA MKOA AMTAKA MKANDARASI KUONGEZA KASI YA UJENZI |Shamteeblog.

Na Muhidin Amri, Songea
MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas, amemtaka mkandarasi wa kampuni Associates LTD kuongeza kasi ya ujenzi wa barabara ya Matomondo hadi Mlale JKT, inayojengwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea.

Kanal Laban ametoa agizo hilo, alipotembelea na kukagua ujenzi wa barabara hiyo ambapo Serikali imetoa shilingi bilioni 4 kupitia fedha za Tozo ya mafuta kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa kilomita 3.5 za lami na ujenzi wa barabara ya changarawe kilomita 19.0.

Kanali Laban alisema, Rais ametoa zaidi ya bilioni 2 kwa ajili ya ujenzi kipande cha barabara ya lami nyepesi urefu wa kilomota 3.5 ili kuwaondolea wananchi changamoto mbalimabali za usafiri hasa wakati wa masika.

"ninazungumzia ujenzi wa kipande hiki cha lami sababu itakuwa mkombozi kwa wananchi hawa, lakini ni wajibu wetu sisi kama wataalamu kuhakikisha tunasimamia miradi ili ikamilike kwa wakati”,alisema.

Aidha,amemtaka Mkandarasi kuongeza kasi ya ujenzi wa barabara hiyo na kuhakikisha anajenga kwa kiwango kinachotakiwa kwani mkataba wa ujenzi huo unatarajia kukamilika tarehe 14 /12/2022 na kuwaomba Wananchi kulinda ujenzi huo wa Barabara hiyo.

Naye Meneja wa Tarura Mkoa wa Ruvuma Wahabu Nyamzungu alisema, mradi huo umefikia asilimia 65 za utekelezaji wake.

“Tarura imeingia mkataba wa ujenzi wa barabara ya Matomondo-Mlale JKT na mkandarasi BR/ ASSOCIATES kwa gharama ya shilingi Bilioni 4, Mkataba ulianza tarehe 14/04/2022 na unatarajia kumalizika tarehe 14/12/2022”alisema Nyamzungu.

Alieleza kuwa, Tarura itaendelea kumsimamia mkandarasi ili kuongeza kasi ya utekelezaji wa mradi hasa kipindi cha kiangazi na kufanya mapitio ya mkataba yanaendelea ili kuwezesha ujenzi wa kalavati, boksi na tabaka la CRS unafanyika kwa wakati.

Katibu wa chama cha mapinduzi kata ya Matomondo Agnes Ngonyani,amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa jitihada za kuwaboreshea barabara hiyo amaboyo kukamlika kwake itafungua fursa kama kukuwa kwa mzunguko wa biashara na usafiri wa uhakika.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas kulia, akimpa maelekezo mkandarasi wa kampuni Associates LTD kuhusu kuongeza kasi ya ujenzi wa barabara ya Matomondo hadi Mlale JKT, wakati alipotembelea na kukagua ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 22.5.
Muonekano wa mradi wa ujenzi wa barabara ya lami nyepesi inayojengwa kwa urefu wa kilomta 3.5 Matomondo hadi Mlale JKT hapa ndipo ulipofika ambapo unatekelezwa kwa fedha za Tozo za mafuta zaidi .




By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post