US, Korea Kusini: Tupo tayari kujibu chokochoko |Shamteeblog.

Meli ya kubeba ndege zinazotumia nguvu za nyuklia ya ‘USS Ronald Reagan’imeweka kambi karibu na mpaka wa Korea Kusini kwa ajili ya mazoezi ya pamoja ya kijeshi ili kukaa ‘mguu sawa’ kwa chochote kinachoweza kufanywa na Korea Kaskazini.

Marekani na Korea Kusini wameanza mazoezi ya siku mbili yenye lengo la kuimarisha uwezo wa kiulinzi wa mataifa hayo mawili katika kile kinachoonekana kujiandaa na uchokozi wowote utakaofanywa na Korea Kaskazini.

Wakuu wa vyombo vya ulinzi wa Marekani na Korea Kusini kwa pamoja wamesema kuwa wapo tayari kwa chochote kitakachotokea.

“Tutaendelea kuimarisha uwezo wetu wa kiutendaji kwa mazoezi ya pamoja na utayari wa kujibu ‘chokochoko’ zozote za Korea Kaskazini ,” wamesema kwa vyombo vya habari.

Kundi la wanamaji la Marekani tayari lilikuwa limeshiriki katika mazoezi ya ulinzi wa makombora na meli za kivita kutoka Japan na Korea Kusini kufuatia Korea Kaskazini kurusha kombora ambalo liliruka sehemu ya Japan.

Siku ya Alhamisi, Korea Kusini nayo ilirusha makombora mengine mawili ya masafa mafupi na baadaye kurusha ndege nane za kivita na nne za mabomu zikiwa zimepangwa umbali wa kilomita kadhaa kutoka mpaka wa Korea Kaskazini.

The post US, Korea Kusini: Tupo tayari kujibu chokochoko appeared first on KITENGE BLOG.



By Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post