Na mwandishi wetu, Arusha
WAKULIMA Mkoa wa Arusha wameshauriwa kufanya uzalishaji wa vyakula wenye lishe bora utakaokidhi afya ya mwananchi baada ya uzalishaji huku wakitakiwa pia kuzalisha chakula cha kutosha kwa ajili ya familia na sio kujali mosoko tu.
Hayo yameelezwa na Rose Mauya Ofisa Lishe Mkoa wa Arusha wakati katika maadhimisho ya Siku ya ya Chakula Duniani ambayo kwa mkoa wa Arusha wameadhimishwa Oktoba 18,2022 ndani ya makao makuu ya Shirika linalohusiana na utafiti wa mboga na matunda(world vegetables center)lililopo Tengeru mkoani Arusha hapa.
Mauya amewataka wakulima kufanya uzalishaji unaotosheleza na chakula ambacho kina lishe na nutrition iwepo kwenye chakula hicho kwani kumekuwa na uhaba wa chakula kwakuwa chakula kingi kinachokizalisha kimeelekezwa kwenye masoko tu.
" Wakati tunajua siku zinavyozidi kwenda tuna ongezeka ,watoto wanakuwa na wengine wapo shuleni ,hivyo aliwahasa wakulima Wanapo zalisha warudi kwenye jadi zetu za kuzalisha vyakula Kwa ajili ya biashara pamoja na vyakula vyetu katika familia zetu
"Tunaona kwamba kunawimbi kubwa Sasa watoto wanapata shida katika lishe wanapata shida kwanini?Kwa vile vyakula tunavizalisha lakini utumiaji au matumizi sahihi ya vyakula hawayafati hivyo tunawaambia wakulima wetu Wanapo zalisha pia wazingatie matumizi sahihi ya vyakula Ili vyakula hivyo vitumike Kwa ajili ya kutuongezea kipato lakini pia katika ujengaji wa afya zetu ili ziweze kuimarika,"amesema Mauya
Aidha amefafanua hali ya lishe kwa Mkoa wa Arusha inaendelea kuimarika na kwamba tatizo kubwa la udumavu lililokuwa linasumbua ,yaani la mtoto kukua kwa kuongezeka kwa umri lakini kimo akiongezeki limepungua kitaifa tupo kwa asilimia 32 lakini kimkoa wapo asilimia 25.Utafiti uliofanyika mwaka huu ukitoka utaonyesha hali hiyo imepungua zaidi
Kwa upande wake Meneja wa Kanda ya Kati wa benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB)Voda's Mwanakatwe amesema wao kama mdau sekta ya kilimo walianzishwa Serikali kuhakikisha kunautoshelevu wa chakula.
Pia kuhakikisha sekta ya kilimo inakuwa kutoka kwenye kilimo cha kujikimu kwenda kwenye kilimo cha biashara wakati malengo yakiwa kuhakikisha uzalishaji unaongezeka na unakuwa na tija.
" Moja ya changamoto ni upotevu wa mazao baada ya mavuno ambapo ripoti zinaonesha chakula kinapotea kati ya asilimia 10 hadi asilimia 30,hivyo tutahakikisha tunaweka mikakati kwenye uhifadhi wa chakula.Pia tumekuwa tunawekeza zaidi kwenye kuongeza thamani kwenye mazao " amesema Mwanakatwe
Baadhi ya wananchi waliohudhuria maadhimisho hayo wakifuatilia uzinduzi
By Mpekuzi
Post a Comment