Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kabla hajaondoka nchini Oktoba 23, 2022, kwenda Korea ya Kusini kwa ziara ya kikazi. Kulia ni Mkewe Mary Majaliwa, wa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Heri James na wa tatu kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam kabla hajaondoka nchini Oktoba 23, 2022, kwenda Korea ya Kusini kwa ziara ya kikazi. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Heri James na wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kabla hajaondoka nchini Oktoba 23, 2022, kwenda Korea ya Kusini kwa ziara ya kikazi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
*****************
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameondoka nchini leo (Jumapili, Oktoba 23, 2022) kwenda Seoul, Jamhuri ya Korea kwa ziara ya kiserikali ya siku tatu.
Akiwa Korea Kusini, Mheshimiwa Majaliwa atakutana na Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Mheshimiwa Han Duck-soo. Pia anatarajiwa kushiriki kongamano la biashara na kukutana na wamiliki wa makampuni makubwa na wenye viwanda. Vilevile, atakutana na Watanzania waishio Korea Kusini.
Kupitia vikao hivyo, Tanzania inatarajiwa kuimarisha mahusiano na Korea Kusini ambayo yamedumu kwa miaka 30. Vilevile, kukuza mahusiano ya kibiashara na uwekezaji, kuangalia fursa za kukuza uchumi wa bluu, utalii, mahusiano ya anga na ushirikiano kwenye sekta ya sanaa na utamaduni.
By Mpekuzi
Post a Comment