Na Jane Edward, Arusha
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaalika wawekezaji kuja kuwekeza nchini kwenye sekta ya utalii, kwa sababu ni nchi yenye amani na utulivu na watu wenye ukarimu.
Akizungumza jijini Arusha kwa niaba ya Rais Samia Hassan Suluhu, Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa wakati akifungua mkutano wa 65 wa Shirika la Utalii Duniani (UNWTO) Kamisheni ya Afrika, wenye kauli mbiu ya "Kujenga upya ustahimilivu wa utalii wa Afrika kwa ajili ya maendeleo jumuishi ya kijamii na kiuchumi," alisema Tanzania licha ya amani na utulivu pia ina maeneo mengi ya uwekezaji.
Amesema uamuzi wa UNWTO kuipa Tanzania mwenyeji wa mkutano huo ni sahihi na umekuja wakati muafaka ambao nchi ina rasilimali nyingi za utalii ambazo wamekaribishwa kuzitembelea na kufurahi.
Aidha amesema Tanzania nchi yenye vivutio vingi na maeneo mengi hivyo kuja kwa wawekezaji nchini kutatoa fursa zaidi kiuchumi.
Akizungumzia Kuhusu upandaji miti alisema uamuzi wa Katibu Mkuu Mtendaji wa UNWTO, Zurab Pololikashvili kuongoza japo la washiriki wa mkutano huo kupanda miti ni mnzuri kwani unaunga juhudi za Tanzania kwenye utunzaji wa mazingira.
Amebainisha kuwa kabla ya janga la Uviko-19 kuingia nchini mwaka 2019 Tanzania iliingiza dola za Kimarekani bilioni 2.6 zilizotokana na sekta ya utalii na kuchangia ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja milioni 1.5
Aidha alisema kwa mwaka 2022 takwimu zinaonyesha sekta ya utalii inabidi kuimarika zaidi hususani baada ya uzinduzi wa programu maalum ya Rais Samia Hassan Suluhu ya The Royal Tour ambapo mapato yatokanayo na utalii yameongezeka kwa asilimia 81.8 kutoka Dola za Kimarekeni milioni 714.59 mwaka 2020 na kufikia Dola za Kimarekani bilioni 1.3 mwaka 2021.
Pia alisema Tanzania baada ya janga hilo imeendelea kufanya jitihada mbalimbali za kufufua sekta ya utalii, ikiwemo utengenezaji wa Filamu ya The Royal Tour iliyoongeza mapato na watalii nchini.
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Pindi Chana alisema mkutano huo umehudhuriwa na mawaziri zaidi ya 33 kutoka nchi wanachama wa UNWTO ukanda wa Afrika wenye dhamana ya utalii masuala ya Utalii na Mali
Alisema mkutano huo utajadili masuala mbalimbali ikiwemo mstakabali wabustawi wa Maendeleo ya sekta ya utalii barani Afrika haswa baada ya athari za UVIKO 19 uliokuwa umeathiri sekta ya utalii Kimataifa kwa wastani wa asilimia 50 hadi 85 katika nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania.
Alisema mkutano huo pia utahusisha wadau mbalimbali wakiwemo wataalam wabobezi wa utalii kwenye vitengo vya ukarimu katika ngazi ya kimataifa na kikanda,watoa huduma mbalimbali katika mnyororo wa utalii,uwekezaji pamoja na watu mashuhuri zaidi ya 50".
"Lengo la ujio wa wabobezi hawa waliobobea katika sekta ya utalii ni kuwapa semena wadau wa sekta ya utalii hapa nchini katika masuala yote muhimu yanayohusu sekta hiyo kuanzia kwenye masoko,fursa, ukarimu pamoja na mwenendo mzima wa kukuza sekta hiyo hapa nchini".
Kwamujibu wa Balozi Pindi alisema mkutano huo utawajengea uwezo wadau wa sekta ya utalii hapa nchini katika kutangaza utalii,kuendeleza na kufungamanisha mazao ya utalii katika kanda mbalimbali za utalii nchini kulingana na shabaha ya nchi kuongeza idadi ya watalii kufikia milioni tano ifikapo mwaka 2025 na pato la Taifa Dolla za Kimarekani Bilioni sita.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akihutubia katika mkutano wa shirika la utalii duniani kamisheni ya Afrika.
By Mpekuzi
Post a Comment