Na Mwandishi Wetu Dodoma
Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (DPP) imekabidhi Wizara ya Fedha na Mipango mali 8,188 zenye thamani ya billion 4.4 zilizotumika kutenda uhalifu mbalimbali nchini.
Akizungumza katika Hafla ya makabidhiano ya mali zitokanazo na uhalifu kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka leo oktoba 3.2022 jijini Dodoma,katibu mkuu wizara ya fedha na Mipango Emmanuel tutuba ametoa wito kwa watanzania kuzingatia sheria na kutojiingiza kwenye vitendo vya kihalifu kwani vinaweza kuhatarisha Maisha yao na utajiri wao.
"watanzania zingatieni sheria na msijiingize kwenye vitendo vya kihalifu maana sheria ipo wazi na kama umetoa gari kumpa mtu ufahamu linaenda kutumika kwa shughuli gani na lisije kutumika kwenye vitendo viovu badae likakuletea hasara" Amesema Tutuba.
sambamba na Hayo Tutuba amesema baada ya kukabidhiwa mali hizo watafanya uchambuzi kuona zinazofaa kwa ajili ya matumizi ya Serikali na watazigawa kwa taasisi za umma zikaendelee kutoa huduma mbalimbali za kijamii na zingine zitapigwa mnada.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mashtaka kutoka ofisi ya Taifa ya Mashtaka sylvester Mwakitalu amesema kuwa mhalifu hatakiwi kupata fursa ya kunufaika na Mali alizozipata kwa uhalifu kwani Mali hizo zikibaki kwa wahalifu zitatumika kufadhili uhalifu mwingine.
"Mali hizi zikibaki kwa wahalifu zitaionesha jamii kwamba uhalifu unalipa,tumehakikisha kwamba Mali zote ambazo zimepatikana kwa njia ya uhalifu zinataifishwa ili kumnyima fursa mhalifu" Amesema Mwakitalu.
Akitoa Taarifa fupi ya uhakiki na uthamini wa Mali zilizokabidhiwa na ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa wizara ya fedha na Mipango Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Mali za Serikali, Chotto Sendo amesema makabidhiano hayo yanahusu nyumba 19, viwanja (9), mashamba mawili (2), vyombo vya moto (63), magari 31 na pikipiki (9) Nyingine ni mbao (4,796), madumu (109) ya lita 20 kila moja ya mafutaa ya ndege/taa, mashine moja ya kukobolea mpunga na madini bati yenye uzito wa kilo 2,104.
Ofisi ya Taifa ya Mashtaka imeanzishwa kama Ofisi huru ya Umma kupitia Tangazo la Serikali na 49 la Mwaka 2018 la tarehe 13 February 2018 la kuanzisha Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa ajili ya kutekeleza Mamlaka ya kikatiba aliyopewa Mkurugenzi wa Mashtaka ya kusimamia haki jinai kwa Mujibu wa Ibara ya 59B ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977.
By Mpekuzi
Post a Comment