Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso Leo tarehe amefika ofisi za RUWASA sehemu ya uchimbaji visima na ujenzi wa mabwawa (DDCA) na kutoa maelekezo mahususi kwa Taasisi hiyo kwa kushirikiana na Bonde la Wami/Ruvu kuainisha maeneo yenye uwezekano wa kupata maji chini ya ardhi na visima vya dharura vichimbwe haraka katika kupunguza changamoto ya Maji.
Mhe Aweso ameagiza Visima vilivyochimbwa miaka ya nyuma 197 vifukuliwe na kukaguliwa/kuboreshwa viweze kutumika kwa kipindi hiki.
Aweso ameitaka DAWASA kuvikarabati Visima vya dharula vilivyochimbwa miaka ya nyuma pamoja na visima vitakavyochimbwa na DDCA baada ya kuanishwa na Wami/Ruvu kuviunganisha kwenye mfumo wa Usambazaji wa Maji wa Dar es salaam kwa ajili ya kuongeza kiasi cha Maji.
Mhe. Waziri Juma Aweso amekagua na kuagiza Mashine mpya za kuchimbia Visima kuanza kutumika kwa dharura hata wakati ratiba ya uzinduzi rasmi nchi mzima na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiendelea kupangwa.
Waziri Aweso ameelekeza matumizi ya dharura ya Mitambo mipya na ile iliokuwepo na kuzitaka Taasisi za Wizara ya maji kufanya kazi kwa ushirikiano kuleta suluhusho la haraka la upatikanaji wa Maji Kwa wakazi wa Dar es salaam.
Awali Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa alitembelea visima vikubwa vya maji mengi Kigamboni na kuruhusu rasmi maji lita milioni 70 kuongeza hali ya uzalishaji Maji maeneo ya katikati ya Jiji la Dar es Salaam na Kigamboni.
By Mpekuzi
Post a Comment