Kwenye headlines za nominations Grammy Awards 2023 ni African Giant Burna Boy tena anayesimama kibabe na kuifanya Africa ijivunie yeye ikiwa ni baada ya kutajwa kama mmoja kati ya wanao wania vipengele vyote viwili vya Global Music kwenye tuzo hizo msimu wa 65.
Ni Last Last ndio ambayo imemuweka kwenye category ya Best Global Music Performance wakati Album ya Love Damini ikiwania Best Global Music Album.
Kwenye kabati la vitu vya thamani Burna Boy anayo tuzo ya Grammy aloikwarua mwaka 2021 kupitia Album yake ya Twice As Tall.
Kutoka Africa, Wasanii wengine walokula mashavu kwenye kuwania Tuzo za Grammy 2022 ni Eddy Kenzo wa Uganda, Angelique Kidjo wa Benin, Wouter Kellerman, Zakes Bantwini na Nomcebo Zikode wa South Africa. •
from Author
Post a Comment