KISHINDO! KANISA LA AGGCI SASA RASMI |Shamteeblog.

*Msajili awapa kibali, CPCT nao watoa baraka zao.

ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Assemblies of God Gospel Church International (AGGCI), Dr. Asumwisye Mwasabila ameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuendelea kuisimamia amani ya nchi na kutoa uhuru wa kuabudu Kwa watanzaia.

Askofu Mwasabila ameyasema hayo leo Novemba 5,2022 akiwa kanisani kwake jijini Mbeya, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuishukuru serikali baada ya kukubali kulisajili Kanisa hilo la AGGCI.

"Namshukuru sana Rais Samia Suluhu Hassan wala hakunibuguzi chochote wakati wa matatizo yangu na kanisa...........,mimi nasema sitaihasi serikali yangu Kwa neema hii niliyoipata", amesema Askofu Mkuu Dkt. Mwaisabila.

Ameongeza Kanisa limefika mahali hapo lilipo leo na kupata katiba hiyo kwa ajili ya serikali kumuheshimu na kwamba anaenda kuwatangazia wakristo, wachungaji na wainjilisti na watu wote tumepata katiba ya Kanisa hili.

Hivyo nawaomba wachungaji mliopewa kibali hiki na katiba hii, asiwepo mtu mwigine akainuka tofauti na wenzake na wasihi fanyeni kazi ya Mungu kama serikali ilivyotuheshimu. Nataka kuliona Kanisa limesimama vizuri. Na kuhusu uchaguzi mkuu wa kanisa, Askofu Dkt. Mwaisabila amesema ataitisha uchaguzi mkuu baada ya kulio na kanisa kuwa limesimama vizuri.

Pia ameliombea taifa la Tanzania lisiingie katika ukame kutokana na kuchelewa Kwa mvua na mvua isije ya mauaji, inyeshe vizuri watu walime na wapande na wapate vyakula vya kutosha.

Aidha askofu Dkt. Mwasabila amewasisitiza watumishi wote wa dhehebu hilo kufika wote Kahama Novemba 9 na 10 mwaka huu wa 2022 bila kukosa ili waelekezane kwa pamoja kile ambacho serikali imewaelekeza kufanya kwa wakati huu.

Kwa upande wa Katibu Mkuu wa AGGCI, Askofu Dkt. Robert Ngai ametoa wito kwa wachungaji wa kanisa hilo kuwa kwa sasa wanaendelea na maandalizi ya mkutano mkuu utakaofanyika Kahama mkoani Shinyanga Nivemba 9 na 10 2022 na kwamba wanatakiwa kufika huko Novemba 8, 2022.

" Ni kwa ajili ya kupeana mikakati ya kuendesha kanisa letu hili na kupeana maelekezo tuliyopewa na serikali yapi tufanye kwa wakati huu kwa ajili ya kusubiri usajili wa kudumu, amesema.

Naye Mweka Hazina Mkuu wa kanisa hili Askofu Jacobo Chacha amesema mkutano huo utatoa taswira halisi ya jinsi gani watakavyoendesha Kanisa lao na mipaka waliyopewa na serikali na ndio maana wameitisha mkutano huo kwa nchi nzima ili watumishi wote wafike Kahama na kupeane zana za kazi na kuanziasha mshikamano na utumishi katika amani hii Mungu aliyowapatia.


By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post