KMC na Meridianbet Wachangia Ujenzi wa Kituo cha Polisi. |Shamteeblog.

 

KLABU ya KMC, alimaarufu kama "KINO BOYS", kwa kushirikiana na Mdhamini mkuu wa klabu hiyo kampuni ya Meridianbet wametoa msaada wa vifaa vya ujenzi wa kituo cha polisi, kilichopo Mtaa wa Tegeta A ambacho kinaendelea kujengwa ili kutoa msaada wa kiusalama kwa eneo hilo.

Vifaa hivyo vilivyotolewa ni mifuko ya Saruji "Cement" zaidi 50 pamoja na ndoo kubwa za rangi 16 na hivyo kuifanya timu hiyo na kampunia hiyo kuwa ni wadau wa kwanza kufika na kuunga juhudi za ujenzi wa mradi huo ambao unatarajia kuhudumia takribani wakazi 10,000 wa eneo hilo na wa maeneo jirani ambao walikuwa wanataabika kwa kukosa ulinzi wa uhakika.



Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Meridianbet, Matina Nkurlu alizungumzia kile kilichowasukuma kushirkiana na KMC kutoa msaada huo.

"Sisi kama Meridiabet kwa kushirikiana na timu ya KMC, tumetoa msaada huu wa zaidi ya mifuko 50 ya saruji 'Cement' pamoja na ndoo kubwa za rangi 17, ili kuunga juhudi za Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan za kuimarisha usalama wa raia na mali zao, hivyo tunaunga juhudi za ujenzi wa kituo hiki cha polisi.





“Pia niwaombe wadau mbalimbali waige mfano huu wa Meridianbet ambao inakuwa kampuni ya kwanza kufika hapa kutoa msaada, na ndio kampuni namba moja pia kwa michezo ya kubashiri hapa Tanzania, nao waguswe kuchangia maendeleo kama haya"-Matina Nkurlu.

Nae Inspekta Henry Mdalingwa ambaye alimwakilisha OCD wa polisi wilaya ya kimara, alipendezwa na hatua hiyo iliyofanywa na Klabu ya KMC kwa Kushirikiana na Mdhamini mkuu kampunia ya Meridianbet.



"Tunawashukuru Klabu ya KMC pamoja na Meridianbet kwa msaada huu ambao unaunga juhudi zilizoanzishwa, ili kuimarisha ulinzi na usalama wa wananchi wote.

"Wananchi wa Tegeta wamekuwa ni wengi, tunahitaji kuwa na usalama wa kutosha ili shughuli za kuijenga nchi ziendelee vizuri, niwakaribishe wadau wengine wajitokeze kama jinsi walivyojitoa Meridianbet"- Inspekta H. Mdalingwa.

Aidha Mwenyekiti wa Mtaa wa Tegeta-A Marco Vaginga, ambao ujenzi wa kituo hicho unafanyika, hakuwa na mengi ya kusema zaidi ya kuwaombea KMC pamoja na Meridianbet wazidi kufanikiwa zaidi.

"Kwa niaba ya wananchi na wakazi wa eneo hili, nawashukuru kwa msaada huu, sina cha kuongea ila nawaombea kwa Mwenyezi Mungu atawaongezea kwa hiki mlichokitoa, nasisitiza kwamba nawashukuru sana, kwa kutimiza kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kazi iendelee"

Meridianbet ni kampuni inayojihusisha na michezo ya kubashiri kwa zaidi ya miaka 10 sasa hapa Tanzania, mbali na michezo ya kubashiri pia wanaendesha michezo ya kasino mtandaoni yenye michezo mingi pendwa kama vile Aviator, Poker, Roulette ambayo ni rahisi kucheza. Pia ukibashiri kwa kitochi unaweza kujishindia zawadi nyingi kama Simu, TV n.k. Beti sasa na Meridianbet kuelekea michuano ya kombe la dunia wanatoa Machaguo Spesho na yenye odds kubwa.




from Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post