NA VICTOR MAKINDA: LIWALE
Kijiji cha Nambinda kilichopo wilaya Liwale Mkoani Lindi,
ni miongoni mwa vijiji 41 nchini vilivyotekeleza mradi wa
kuhifadhi misitu kwa kuwezesha biashara endelevu ya
mazao ya misitu Tanzania (CoForEST), unaotekelezwa na
Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG) kwa
kushirikiana na Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu
Tanzania (MJUMITA) chini ya ufadhili wa Shirika la
Maendeleo na Ushirikiano la Uswisi (SDC).
Kutokana na biashara endelevu ya mazao ya misitu,
mapato yaliyopatikana yamewawesha wananchi wa kijiji
hicho kuanza ujenzi wa zahanati unaotarajiwa kugharimu
kiasi cha Shilingi milioni 125 ambapo mpaka sasa tayari
wametumia Shilingi Milioni 33 kwenye ujenzi huo.
Akizungumza na timu ya waandishi wa habari waliofika
kijijini hapo kwa lengo la kujionea matokea yaliyotokana
na mradi wa CoForEST,
Mwenyekiti wa kijiji hicho Said Koe, alisema kuwa moja ya changamoto kubwa inayowakabili kijijini hapo ni ukosefu wa huduma za afya hivyo fedha walizokusanya kutokana na biashara endelevu ya mazao ya misitu wameamua kuanza ujenzi wa zahanati ili kuepukana na adha ya ukosefu wa huduma za afya.
“ Tunalishukuru sana shirika la TFCG na MJUMITA kwa
kutuletea mradi huu wa CoForEST kwa kuwa sasa tunakwenda
kujikomboa kutoka kwenye changamoto kubwa ya kufuata
huduma ya afya zaidi ya kilometa nane kutoka kijiji hapa”. Anasema Koe.
Koe anaongeza kusema kuwa akina mama wajawazito na
watoto wamekuwa wahanga wakubwa wa kukosekana kwa
huduma za afya kijijini hapo hivyo mara baada ya mradi wa
CoForEST kufika kijijini mwaka hapo na kuelekezwa namna ya
kuihifadhi na kuvuna mazao ya msitu wao wa asili kwa njia
endelevu wameitumia asilimia 48 ya mapato yao kujenga
zahanati ya kjiji.
Koe anaongeza kusema kuwa ujenzi huo wa zahanati umefikia
kwenye ngazi ya lenta hivyo wanaiomba serikali kuwasaidia
kumalizia hatua zilizobaki.
Akisoma taarifa ya mafanikio ya Mradi wa CoForEST kijijini
hapo, Katibu wa kamati ya maliasili, Said Barabara, alisema
kuwa tangu waliopoanza mavuno endelevu ya mazao ya msitu
wao wa kijiji, katika msimu wa mwaka 2021-2022
wamekusanya jumla ya Shilingi 60.9 Milioni ambazo
wanazilekeza kwenye shughuli za maendeleo na ulinzi wa
misitu.
By Mpekuzi
Post a Comment