*********
Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka umekuwa kivutio baadhi ya nchi ya Afrika kuja kujifunza na wengine kutaka nchi zao kuwa na uwekezaji huo.
Hayo ameyasema Mkurugenzi wa Fedha na Maendeleo ya Biashara wa DART Deus Kasmir kwa Niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa wakati DART walipotembelewa na Makatibu Wakuu wa Serikali za Mitaa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliofika kujionea huduma za usafiri wa Umma uendeshwa katika jiji la Dar es Salaam.
Kasmir amesema kuwa mradi wa mabasi yaendayo haraka kwa sasa ndio unakuwa na unatembelewa na mataifa mbalimbali namna wanavyoweza kutoa huduma ya usafiri unaofanya kuchochea uchumi wa nchi kutokana wananchi kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
Amesema kuwa wakati wakitembelea mifumo DART wanapata picha namna wanavyodhibiti fedha kupitia mifumo hiyo ambapo imeonesha Tanzania imepiga hatua kwenye mifumo ya kieletroniki kwa serikali kujua mapato yake.
Aidha amesema kuwa ziara ya Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wameonesha baadhi ya nchi kuja kujifunza na kwenda kutekeleza nchini mwao katika kutoa huduma za usafiri wa Umma kwa wananchi.
Hata hivyo amesema kuwa licha ya kuwa kivutio wakala unaendelea kuboresha huduma za usafiri pamoja ba mifumo mbalimbali kutokana na teknolojia inabadilika kila siku.
"Mradi wa Mabasi umekuwa kivutio kazi yetu DART ni kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi kwani hicho ndio kipaumbele chetu na tunasimama kwenye hicho kipaumbele hicho"amesema Kasmir.
By Mpekuzi
Post a Comment