Muonekano wa Jengo Jipya la Hospitali ya Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja linalojengwa katika eneo la Lumumba Wilaya ya Mjini Unguja, likiendelea na ujenzi wake katika hatua za mwisho za ujenzi huo
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika jengo la Hospitali ya Mkoa wa Mjini Magharibi, wakati wa ziara yake leo 19-11-2022, kutembelea ujenzi huo na kujionea hatua iliyofikia na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Wilaya ya Mjini Unguja.Mhe. Rashid Simai Msaraka.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akitembelea Ujenzi wa Hospitali ya Mkoa wa Mjini Magharibi inayojengwa katika eneo la Lumumba Wilaya ya Mjini Unguja, akiwa katika ziara yake kutembelea ujenzi huo na kujionea hatua iliyofikia.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akipata maelezo ya maendeleo ya Ujenzi wa Hospitali ya Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, kutoka kwa Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui, inayojengwa katika eneo la Lumumba Wilaya ya Mjini Unguja, wakati wa ziara yake kutembelea ujenzi huo leo 19-11-2022.
.(Picha na Ikulu)
By Mpekuzi
Post a Comment