Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV
TUNAKWENDA kuandika historia mpya! Ndivyo unavyoweza kuelezea baada ya Serikali kusaini makubaliano na Benki ya Dunia ya mkopo nafuu wa Sh. Trilioni 1.24 ambazo zitatumika katika ujenzi wa daraja jipya la kisasa eneo la Jangwani pamoja na mradi wa umeme vijijini.
Kujengwa kwa daraja la Jangwani unaelezwa kwamba Tanzania inakwenda kuaandika historia nyingine ya daraja bora na la aina yake, linakwenda kuwaondoa wakazi wa maeneo hayo na Dar es Salaam kwa ujumla kwenye changamoto ya mafuriko ambayo imekuwa ikitokea inapofika msimu wa mvua.
Waziri wa Fedha na Mipango Dk Mwigulu Nchemba ameeleza hayo leo Novemba 21 mwaka 2022 Bada ya kuingiwa kwa makubaliano hayo kati ya Serikali ya Tanzania na Benki ya Dunia iliyoamua kutoa mkopo nafuu unaokwenda kutekeleza miradi hiyo miwili.
"Mikataba hii miwili yenye thamani ya dola milioni 535 sawa na Sh trilioni 1.24 itaandika historia na kukuza uchumi wa nchi.Na hapa nieleze kwamba huu ni mwanzo tu kati ya yale mambo makubwa yanayokwenda kufanywa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.Kwa mwaka huu wa fedha anakwenda kufanya ujenzi wa miradi itakayoandika historia."
Akizungumza kuhusu miradi hiyo Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Rogatus Mativila, amesema daraja la kisasa linalokwenda kujengwa Jangwani muonekano wake utakuwa kama daraja la Tanzanite ambalo linapita katika Bahari ya Hindi au daraja la Kigamboni.
" Ujenzi wa daraja hili utakapokamilika unakwenda kuondoa kabisa mafuriko ambayo yamekuwa yakisababidha adha kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam.Ujenzi wa daraja la Jangwani utakuwa daraja la mita 390 na litainuka kwa mita sita.Pia ujenzi utahusisha upanuzi wa mto kwa kilometa 1.8 chini, kutakuwa kingo za zege,"amefafanua.
“Ujenzi utagharimu zaidi ya dola milioni 63.3 na hivi karibuni tunatarajia kutangaza tenda ambapo baada ya miezi mitatu hatua za awali zitakuwa zimekamilika,”amesema na kuongeza usanifu wa ujenzi tayari umekamilika na ujenzi utakamilika baada ya miaka mitatu.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini, Bw. Nathan Belete (kushoto), wakiwaonesha wanahabari, mikataba ya mikopo nafuu ya dola za Marekani milioni 535 sawa na shilingi trilioni 1.24, kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo. Kulia ni Waziri wa Nishati Mhe January Makamba akishuhudia tukio hilo.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba na Mwakilishi MKazi wa Benki ya Dunia nchini, Bw. Nathan Belete (kushoto), wakisaini mikataba ya mikopo nafuu ya shilingi trilioni 1.24 kwa ajili ya miradi miwili ukiwemo Mradi wa REA na Mradi wa kukabiliana na mafuriko katika Bonde la Mto Msimbazi. Anayeshuhudia ni Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba.
Mtendaji Mkuu wa Tanroads Mhandisi Rogatus Mtivila akitia saini makubaliano ya mkopo wa ujenzi wa daraja la Jangwani kati ya TANROADS na Benki ya Dunia,hafla hiyo imefanyika Novemba 21,2022 jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt,Mwigulu Nchemba pamoja na Waziri wa Nishati Mhe.January Makamba
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini, Bw. Nathan Belete (kushoto), wakiwaonesha wanahabari, mikataba ya mikopo nafuu ya dola za Marekani milioni 535 sawa na shilingi trilioni 1.24, kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo. Kulia ni Waziri wa Nishati Mhe January Makamba.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini, Bw. Nathan Belete (kushoto), wakipongezana mara baada ya kusaini mikataba ya mikopo nafuu ya dola za Marekani milioni 535 sawa na shilingi trilioni 1.24, kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo. Pichani kati ni Mtendaji Mkuu wa Tanroads Mhandisi Rogatus Mtivila akishuhudia.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba akisaliamiana na Mtendaji Mkuu wa Tanroads Mhandisi Rogatus Mtivila mara baada ya hafla fupi ya kusaini mikataba ya mikopo nafuu kuisha.
By Mpekuzi
Post a Comment