TRA Mkoa wa Ilala yatoa msaada Kituo cha Mother Teresa Mburahati |Shamteeblog.

Kaimu Meneja Mkoa wa Kikodi Ilala Masau Clifford Malima akimkabidhi zawadi Mzee Joachim Michael kutoka kituo cha watu wenye Mahitaji Maalum cha Mothe Teresa Mburahati ( Missionay Charity Nyumba ya amani na furaha) katika muendelezo wa siku ya kipindi cha huduma na shukrani kwa mlipa kodi.

Kaimu Meneja Mkoa wa Kikodi Ilala Masau Clifford Malima akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi msaada katika Kituo cha Mother Teresa Kilichopo Mburahati jijini Dar es Salaam.
Mmoja ya wazee katika Kituo cha Mother Teresa Kilichopo Mburahati  Joachim Michael akitoa shukrani Kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Kodi Ilala baada ya kupatia msaada wa vitu Mbalimbali  , jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya mahitaji waliyoto TRA Mkoa wa Ilala kwenye kituo cha Mother Teresa Kilichopo Mburahati jijini Dar es Salaam.

*Yasema ina wajibu wa kutambua makundi ya watu wenye mahitaji maalum

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa kodi Ilala umesema kuwa katika shughuli za ukukusanyaji wa mapato mpaka kufikia Mwezi Oktoba ufanisi wao umefikia Asilimia 104.5 ikiwa ni lengo walilopangiwa.

Akizungumza mara kukabidhi vyakula na Mahitaji Mengine kwa watu wenye mahitaji maalum kwa kituo Mother Teresa Kilichopo Mburahati Kaimu Meneja wa Mkoa wa Kodi Ilala Masau Clifford Malima ....amesema kuwa katika mwaka wa fedha wanatarajia kukusanya zaidi ya Trilioni Mbili ambayo hiyo inatokana na kujipanga kwa kwao ili maendeleo yaweze kuonekana.

Amesema kuwa TRA imetoa msaada huo kutokana na kutambua watu wenye mahitaji maalum ili kuhakikisha nao wanaishi kama watu wengine kwa kuwa na mahitaji yanayomhusu kama binadamu pamoja na kufanya kituo hicho kuendelea kuwepo.

"Sisi tusipotoa misaada ni kufanya kituo cha mothor Teresa kisiwepo kwani wanaohudumiwa kituoni hapo ni watanzania wenzetu ambao wanakabiliwa na changamoto mbalimbali"amesema Malima

Amesema wao kama sehemu ya Jamii wamelazimika kwenda kutoa msaada katika kituo hicho kutokana na kuguswa kuonyesha mchango wao kwa watanzania wenzao na sehemu ya taaisi kutambua mahitaji ya jamii.

"Sisi kama wana Ilala tumeona kwa kipindi hiki tutumie muda huu kutoa shukrani kwa jamii yenye uhitaji ambapo tumekuja kuleta zawadi mbalimbali na tumezikabidhi kwenye uongozi kwani sisi kama Jamii tumeguswa sana"amesema Malima

Malima amesema Mkoa wa Kikodi Ilala wameendela kufanya shughuli zakukusanyaji wa mapato ambapo mpaka kufikia Mwezi Oktoba ufanisi kutokana na maelekezo ya viongozi wa juu pqmoja na kupata ushirikiano kutoka makundi mbalimbali ya walipakodi huku wakitarajia kukusanya Trilionj 1.25 kwa mwaka huu wa Fedha.

Ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa makundi mbalimbali kuhakikisha wanalipa kodi ikiwa ni pamoja na kutumia matumizi ya EFD Ili kuendelea kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato nchini.

Hata hivyo amewataka wananchi kuendelea kuonyesha ushirikiano kwa Mamlaka hiyo Ili waendelee kufanikisha ukusanyaji wa mapato Nchini na kusaidia serikali.

Kwa upande wake Mmoja ya wazee katika kituo hicho Joachim Michael ameipongeza TRA Mkoa wa Kikodi Ilala Kwa kuonyesha kuguswa na kuwasaidia watu wenye uhitaji maalum na kuongeza kuwa msaada huo hautapotea na Mungu atalipa.

Amesema yupo katika kituo hicho miaka Tisa hivyo ameiomba jamii kuonyesha moyo wa kuiga mfano wa TRA wa kuendelea kuisaidia Jamii misaada mbalimbali.


By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post