Na Victor Masangu,Pwani
Mamlaka ya mapato (TRA) Mkoa wa Pwani imeamua kutumia kilele cha maadhimisho ya wiki ya mlipa kodi kuwakutanisha kwa pamoja baadhi ya wafanyabiashara na wawekeza kwa lengo la kuwapongeza na kuwapatia vyeti na tuzo kutokana na kuwa bora katika suala zima la ulipaji wa kodi kwa weledi.
Meneja wa TRA Mkoa wa Pwani Emmanuel Maro ameyabainisha hayo wakati wa halfa hiyo ambayo ilifanyika Wilayani Kibaha na kuwashirikisha viongozi mbali mbali wa serikali pamoja na wafanyabiashara na wawekezaji kutoka wilaya zote saba za Mkoa.
Maro alibainishwa kwamba lengo lao kubwa ni kuweka mikakati madhubuti kwa ajili kuweza kuwafikia walenga ambao ni walipa kodi na kuwapatia elimu ambayo itawasaidia katika kufahamu umuhimu wa kulipa Kodi bila kutumia mabavu.
Aliongeza kwamba wao Kama TRA waliona kuna umuhimu mkubwa wa kutoa zawadi ya vyeti na tuzo kwa wafanyabiashara hao na wawekezaji kwa kutambua mchango wao katika kuchangia pato la Taifa kwa lengo la kuwaletea wananchi maendeleo.
"Sisi Kama TRA tumeamua katika kuadhimisha wiki hii ya mlipa kodi tufanye shughuli mbalimbali za kijamii ikiwema kuona umuhimu wa kuwakutanisha wadau wetu ambao wamekuwa mstari wa mbele katika suala zima la ulipaji wa kodi kwa wakati,"alisema Maro.
Katika hatua nyingine alisema pamoja na kutekeleza majukumu yao ipasavyo lakini wanakabiliwa na chsngamoto ya baadhi ya wafanyabiashara kutokuwa waaminifu kutokana na kukwepa kubadilika na kutoa risiti kwa mfumo wa kielekitroniki.(EFD)
Kwa upande wake Naibu kamishina wa TRA nchini Jofrey Kitundu amesema kwa Sasa wameweka mipango madhubuti ambayo itasaidia kwa kiasi kikubwa katika ukusanyaji wa kodi katika maeneo mbali mbali kwa msumo wa kisasa ambao pia utasaidia kuongeza pato la Taifa.
"Tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutekeleza maagizo matatu yaliyotolewa na Rais wa awamu ya sita Samia Suluhu Hassan kwa kutanua wigo mkubwa wa ukusanyaji wa kodi bila kutumia mabavu pamoja na kutatua changamoto zinazowakabili wafanyabiashara katika maeneo yao,"alisema Kitundu.
Naye mmoja wa wafanyabiashara ambaye ameibuka kuwa mshindi wa jumla kimkoa katika ulipaji bora wa kodi hakusita kuipongeza TRA na serikali kuweka mifumo mzuri ya ulipaji kwa njia ya kieletroniki.
Mamlaka ya mapato (TRA) Mkoa wa Pwani imeweza kuadhimisha wiki ya mlipa kodi kwa kufanya shughuli mbali mbali ikiwemo kutoa msaada kwa jamii pamoja na utoaji wa vyeti na tuzo kwa wafanyabiashara wadogo,wakati pamoja na wale wakubwa.
By Mpekuzi
Post a Comment